Wito
umetolewa kwa wote wanaohusika katika mchakato wa kupata katiba mpya kungalia
maslahi ya Taifa kwanza badala ya kuangalia maslahi binafsi au ya vyama vyao.
Hayo
yamesemwa na afisa wa shirika la Oxfam nafasi za wanawake katika kupata Katiba
Mpya Heri Ayubu wakati wa mdahalo wa mchakato wa katiba na jinsia uliofanyika
Juni 26 na kuwahusisha Wanawake mbalimbali kutoka tarafa ya Kilosa.
Ayubu
amesema tangu kuanza kwa mchakato wa kupata katiba Mpya kumekuwepo na
changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya makundi kuvutia kwake hususani watu wa
vyama vya siasa hali inayotoa mashaka ya kupatikana kwa katiba nzuri
iliyopendekezwa na wananchi.
Aidha ayubu
ameongeza kusema kuwa wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wadau hususani
wanawake ili muda utakapofika wakati wa kupiga kura ya katiba wawe na ufahamu mkubwa ju ya katiba
hiyo maamuzi watakayotoa yawe sahihi.
Kwa upande
wa wajumbe waliohudhulia mdahalo huo mwalimu Sikuzani Mfinanga na Rehema Mhini kwa niaba ya wanawake wenzao
wamesema kuwa wanashukuru kwa kufanyika kwa mdahalo kwani umeweza kuwapanua
kifikra na wamewaomba wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuheshimu mawazo yao na
kutoa wito kwa wanawake nchi kuisoma kwa makini katiba mpya itakapotoka na
kujitokeza katika kuipigia kura.
Mdahalo huo umeandaliwa na shirika la msaada wa
kisheria morogoro Palaregal kwa kushirikiana na mashirika ya Restress
Development,
No comments:
Post a Comment