Wednesday, December 8, 2010

HOSPITALI YA WILAYA NJOMBE (KIBENA) YAKOSA HUDUMA YA X-RAY.

MWEZI WA SABA SASA HOSPITALI YA WILAYA NJOMBE (KIBENA) YAKOSA HUDUMA YA X-RAY.



Zoezi la Kutambua na Upimaji Wagonjwa wa Fistula Wilayani Njombe limeshindwa kufanyika kama ilivyokusudiwa kufuatia Idadi ndogo ya Wananchi waliojitokeza katika Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena

Hadi Kufikia jana wakati wa Kufunga Zoezi hilo ni Mwanamke Mmoja Tu aliejitokeza kupimwa na kugundulika kuwa na Ugonjwa huo ambae Tayari amepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya Matibabu Zaidi

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena Daktari Evarest Mtitu Amesema idadi hio ndogo ya Wananchi waliojitokeza Imetokana na Kuchelewa kufika kwa Taarifa kwa Wananchi juu ya Uendeshwaji wa Zoezi hilo ambalo liliendeshwa kwa siku mbili

Amesema kutokana na Ufinyu wa Bajeti katika Sekta ya Afya Wilayani Njombe Umechangia kutokufanikiwa kwa

Kwa Mwezi wa Saba Sasa Hospitali ya Kibena Wilayani Njombe imeshindwa kutoa Huduma ya Upigaji Picha za X-Ray Kutokana na Kukosa Mtaalamu wa Fani hio

Hali hio imetokana na Mtaalamu Aliekuwepo Awali kupata Nafasi ya Masomo na Kwenda Kusoma Katika Tume ya Taifa ya Mionzi hali ambayo Imesababisha Huduma Hio Kusitishwa

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kibena Daktari James Ligwa Amesema kutokana na Kukosekana kwa Huduma Hio katika Hospitali hio imesababisha Wananchi kulazimika kwenda katika Vituo na Zahanati Binafsi ili kuweza kupata Huduma Hizo Hatua Ambayo Imewasababishia Kuongeza Ugumu wa Maisha Kutokana na Gharama Kubwa katika Vituo Hivyo

Amesema Hospitali ya TANWART na IKONDA zimekuwa Zikitumiwa na Hospitali hio Kama Njia Mbadala ya kusaidia Wagonjwa wanaofikia katika Kituoi Hicho Kwa ajili ya Kuhitaji Huduma Hizo

Akizungumza na mtandao huu Hospitalini hapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hio Daktari Evarest Mtitu Amesema Tayari Wamewasiliana na Serikali kwa ajili ya kuomba Kuajiri Mtaalamu Mwingine ambapo kwa sasa Wanasubiri majibu kulingana na Taratibu za Ajira

No comments:

Post a Comment