Saturday, September 7, 2013

CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH MOROGORO CHAFANYA TAMASHA LA MICHEZO ILI KUBORESHA MICHEZO NA AFYA ZA WANACHUO.



CHUO CHA MTAKATIFU JOSEPH MOROGORO CHAFANYA TAMASHA LA MICHEZO ILI KUBORESHA MICHEZO NA AFYA ZA WANACHUO.

Chuo cha mtakatifu Joseph kilichopo mkoani Morogoro leo  kimefanya tamasha la michezo katika viwanja vya michezo vya chuo cha kilimo (Sua) kwa lengo la kuboresha michezo na afya za wananchuo kupitia michezo .

Michezo hiyo iliyoanza nyakati za asubuhi na kuhitimishwa saa kumi jioni ilihusisha pia wanachuo kutoka katika chuo cha  Morogoro school of journalism (MSJ) ambapo michezo ya mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba ,kukimbiza kuku,na mbio za mita mia nne kwa upande wa wanafunzi na wakufunzi wao kutoa katika vyuo vyote viwili.

Mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya St Joseph Morogoro na Chuo cha habari morogoro(MSJ) Iliyoisha kwa ushindi wa goli 3(MSJ)  kwa 1 St Josep (Picha na Beatrice Majaliwa) 


Tamasha hilo lilokuwa na lengo la kuwaweka wanafunzi katika hali nzuri kiafya ,kufahamiana na kuweka mahusiano na ushirikiano baina ya vyuo shiriki.

Akisoma hutuba kwa mgeni rasmi Rais wa wanachuo  kutoka katika chuo cha Mtakatifu Joseph bwana Emanuel  Kabakeza amesema miongoni mwa chanagamoto wanazokutana nazo katika michezo ni pamoja na upungufu wa vifaa vya michezo ambavyo huwafanya kushindwa kufanya michezo yao kikamilifu.

Akijibu risala hiyo wakati wa kufunga bonanza hilo  mwakilishi wa mbunge wa Morogoro mjini ,katibu wa mbunge huyo bwana Mourice Masala  amesema kwa upande wake amefurahishwa na tamasha hilo lilioandaliwa na chuo hicho na kusema kwa sasa chuo kimekuwa na umuhimu mkubwa katika manispaa ya morogoro.

Masala  amesema kuwa kwa sasa chuo cha mtakatifu Joseph kimekuwa mkombozi kwa vijana wengi  katika mkoa wa morogoro na mikoa mingine kwa ujumla ikiwa ni sehemu mojawapo ya kupata taaluma katika fani mbalimbali.

Katika kupunguza adha ya ukosefu wa vifaa vya michezo ofisi ya mbunge imetoa seti moja ya jezi ya mchezo wa mpira wa miguu na mpira mmoja wa mchezp wa pete kwa wasichana ili kuongeza ari ya michezo kwa wanachuo hao.

No comments:

Post a Comment