Saturday, September 7, 2013

MBUNGE WA MOROGORO MJINI MHESHIMIWA ABDUL AZIZ ABOUD AWATAKA WANAVYUO KUSHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI NA KUEPUKANA NA TABIA HATARISHI



MBUNGE WA MOROGORO MJINI MHESHIMIWA ABDUL AZIZ ABOUD AWATAKA WANAVYUO KUSHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI NA KUEPUKANA NA TABIA HATARISHI

Mbunge wa morogoro mjini mheshimiwa Abdul Aziz Aboud amewataka vijana na wanavyuo waliopo vyuoni kujishughulisha katika michezo ikiwa ni sehemu  mojawapo katika afya ya mwanadamu.

Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo katibu wake Bwana Mourice Masala  amesema kuwa michezo ni muhimu kwa vijana na hasa kwa wale waliopo vyuoni kwani huwafanya kuchangamsha miili yao na kuepukana na kujiingiza katika vitendo viovu mara baada ya masomo yao.

Masala ameyasema hayo wakati akifunga bonanza la michezo lililovishirikisha vyuo vya Mtakatifu Joseph na Chuo cha uandishi wa habari MSJ vyote vya mkoani Morogoro.

Pia amewahasa vijana wanachuo hao waliopo mafunzoni kuzingatia kwa makini mafunzo yao ili waweze kuyahitimu kwa ufanisi na kuachana na tabia mbaya ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya vijana ikiwemo kujjiingiza katika kutumia madawa ya kulevya.
Nao wanachuo hao walionesha ushiriki wao kikamilifu katika kushiriki kwao katika kufanya michezo mbali mbali ambayo baadhi yake ilishirikisha wakufunzi kutoka katika vyuo hivyo.

Na Beatrice Majaliwa
Morogoro

No comments:

Post a Comment