Kituo cha sheria na haki za
binadamu nchini Tanzania LHRC mwishoni mwa wiki iliyopita kimetimiza umri miaka
19 toka kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliohudhulia katika sherehe za kutimiza miaka 19 ya kituuo cha kutetea haki za Binadamu LHRC Jijini Dar es salaam.
Katika sherehe hiyo ya
kusheherehekea miaka 19 toka kuanzishwa kwake yaliyohudhuliwa na mgeni Rasmi
Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania Jaji Joseph Walioba
pamoja na viongozi mbalimbali kwa ngazi za kisiasa na kiserikali.
Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko Jaji Joseph Warioba akiongea wakati wa maazimisho hayo ya 19 ya kituo cha wasaidizi wa kisheria.
Katika sherehe hiyo ya kutimiza
miaka 19 toka lianzishwe shirika hilo la kutetea haki za binadamu Walioba
ameliomba shirika hilo kusimama imara kwa kuhakikisha kila Mtanzania anapata
haki yake stahiki hasa
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi,Helen Kijobi Simba
kipindi hiki cha mchakato wa kupata katiba mpya amesema
kuwa wananchi wanapaswa kutambua katiba ili inapofika wakati wa kuipigia kura
wajue wanaipigia kura katiba ipi.
Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Waroba akifuatiwa na Mkurugenzi wa kituo cha usaidizi wa kisheria Bi,Helen Kijobi Simba akifuatiwa na Askofu
Aidha Warioba amewataka wasaidizi
wa kisheria kuwapa elimu wananchi waliopo vijijini na mjini ili kuhakikisha
wananchi walio wengi wanajitambuana kutambua umuhimu wao katika jamii na Taifa
kiujumla.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria kutoka wilayani Serengeti wakipokea zawadi baada ya utendaji mzuri wa kazi zao
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
shirika hilo la kutetea haki za binadamu nchini Tanzania LHRC Helen Kijobi
Simba amesema kuwa katika utendaji wao wa kazi wakiwa wasaidizi wa kisheria
wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo wanasiasa kuingilia katika utendaji
wao wa kazi na kuonekana wasaidizi wa
Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof;Ibrahim Lipumba[kushoto] akiwa na mmoja na wajumbe katika Tamasha la miaka 19 ya kituo cha sheria na haki za binadamu.
kisheria kama wapinga maendeleo na kuwa
kikwazo jambo ambalo Bi,Simba amesema ni kikwazo kikubwa kwao katika ufanyaji
wa kazi.
Inayoonekana kwa mbele ni keki iliyoandaliwa katika tamasha la kituo cha sheria na haki za binadamu.
Aidha Bi,Simba amewataka
wasaidizi wa kisheria kutokata tamaa katika kutetea haki za wananchi ambao
hawajui hata pakuanzia.
No comments:
Post a Comment