Wednesday, October 1, 2014

KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO ASEMA UJENZI WA MAABARA UTAONDOKA NA MTU MADARAKANI.



Viongozi wa vijiji na kata wametakiwa kusimamia kwa juhudi ujenzi wa maabara tatu za sayansi katika shule za sekondari.
Katibu mkuu wa mkoa wa morogoro aliyevaa suti ya kijivu Elias Ntandu  akitoa maelekezo ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari kutukutuakiwa pamoja na viongozi alioambatana nao katika ziara ya ujenzi wa maabara.

Hayo yamesemwa na Katibu tawala mkoa wa morogoro Elias Ntandu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ziara yake ya kutembelea shule 39 za sekondari katika wilaya ya kilosa ambapo amekagua ujenzi wa maabara katika shule hizo na kujionea hali halisi ambapo amesema kuwa shule nyingi  za sekondari 

              Viongozi wakiwa wanakagua maabara katika shule ya sekondari Mazinyungu iliyopo wilayani kilosa
hazijakamilisha ujenzi huo wa maabara ambalo ni tamko la mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa hadi kufikia mwezi wa kumi na moja 2014 maabara hizo 
Maabara ya Fizikia ambayo inatumika ya shule ya sekondari Mazinyungu iliyopo wilayani kilosa mkoani morogoro.

zinatakiwa kukamilika na kwa viongozi wa kijiji na kata wanatakiwa kukamilisha ujenzi huo mapema ya mwezi wa kumi 2014.
Diwani wa kata ya Mbumi Mama mbaruku akitoa maelekezo kwa viongozi kuhusu ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Mbumi iliyopo katika eneo lake la kiutawala.

Katika ziara hiyo ya kukagua ujenzi wa maabara iliyoambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya kilosa Elias Tarimo,Katibu tawala wilaya Hilary Sagala Afisa mipango wilaya Lwidin Ngakoka 
 Baadhi ya viongozi wakiwa katika shule shule ya sekondari Mvumi kabla ya kwenda kukagua ujenzi wa maabara.
Afisa elimu sekondari wilayani kilosa Jonas Ntigoza pamoja na Afisa elimu Taaluma mkoa Raphael Pagala na 
viongozi wengine kutoka wilayani kilosa ambapo Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka 
Katibu Tawala mkoa wa Morogoro Elias Ntandu akiwa na mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wakiwa wanajumuika katika kuchimba shimo ambalo litatumika pindi maabara itakapokuwa tayari.

viongozi kupiga mahesabu vizuri kughusu ujenzi huo wa maabara ili pindi wanapotoa gharama ya uchangiaji kwa kila mwananchi kusiwe na utata  kwani ujenzi wa maabara unategemea nguvu ya wananchi.
Afisa elimu sekondari Jonas Ntigonza akiwa anaangalia ujenziwa maabara katika shule ya sekondari Gongwe iliyopo mvumi wilayani kilosa.

Aidha Tarimo amewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuingilia shughuli za ujenzi wa maabara kisiasa kwani

                     Maabara ya shule ya sekondari Ludewa iliyokuwa hatua za mwisho za umaliziaji.
 jambo hilo la ujenzi si swala la kisiasa na kuwataka wananchi kujitoa kwa hali na mali ili kukamilisha ujenzi 
huo wa maabara kwa kila shule ya sekondari mapema ya mwezi wa kumi 2014.
Ujenzi wa maabara ukiwa katika ngazi ya uchimbaji wa msingi katika shule ya sekondari Mkulo Iliyopo wilayani kilosa mkoani Morogoro na viongozi wakiwa wanakagua ujenzi huo.


Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo akiwa katika uwajibikaji kwa vitendo kwa kuchimba  msingi katika shule ya sekondari Kutukutu.

No comments:

Post a Comment