Friday, June 30, 2017

WAKULIMA WILAYANI KILOSA WATAKIWA KUJIUNGA NA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUJIPATIA MAENDELEO KWA NJIA YAKUSHILIKIANA

Wakulima wilayani kilosa mkoani morogoro wametakiwa kuvitumia vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na mazazo yao pale wanapohitaji kuyauza.
Hayo yamesema katika mkutano mkuu wa kumi wa chama cha ushirika wilayani kilosa [kilosa co-operative union]KICU na muwakilishi wa mkuu wa wilaya Afisa utumishi mkuu wa wilaya ya kilosa Bw,Emmanuel .T. Nzunda akisoma hotuma iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo ya kilosa Adam Mgoyi na ameviomba vyama vya ushirika kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo na madawa ya mazao yauhakika na ametoa onyo kwa  wakulima kuacha kuchanganya mazao yao na mchanga hasa zao la ufuta kwani kwa kufanya hivyo kunashusha soko la biashara ya mazao na kushusha kipato katika wilaya pia amewahamasisha akina mama kujiunga na vyama vya ushirika ili kuleta chachu ya maendeleo katika sekta ya nzima ya ushirika.
Naye mwenyekiti wa mkutano huo Bw,Thadei Mnhangwi amewahamasisha wanawake,vijana na makundi yote kujiunga na chama cha ushirika ili kujipatia maendeleo kwa njia ya kushirikiana kwa sababu chama hicho kitawasaidia wakulima, kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kuwahamasisha wakulima kujiunga na chama hicho, kwani wataweza kulima kilimo cha mkataba kilimo ambacho kitawasaidia wakulima kumudu gharama za kilimo na kuyauza mazao yao kiurahisi. Ameongeza kwa kusema kuwa kwa miaka hii, vyama vya ushirika vinaonekana kufifia na vingine kufa kwa sababu ya vyama hivyo kuingiliwa na siasa na kuwepo kwa soko hulia pia amewataka wakulima kuyatunza mazao yao vizuri mara baada ya kuyavuna ili kukuza soko la biashara ya mazao na kuyauza kupitia vyama vya ushirika ili kuwa na Takwimu kamili ya mazao yaliyouzwa.
Kwa upande wake meneja wa viwanda vya pamba vya ushirika wilayani kilosa Bw,Mohamedi Kindwiku amewaomba wakulima kujihusisha na kilimo cha pamba kwa kuwatia moyo kuwa kiwanda hicho kipo wilayani kilosa na mashine zipo.
Aidha Afisa kilimo Abel A.mchome aliyemwakilisha Afisa ushirika wilaya amewataka wanachama hao wao kuwa mstari wa mbele katika kilimo ili wawe mfano mzuri kwa wanachama wanaotakiwa kujiunga na ameahidi kutoa ushirikiano katika kuliendeleza shirika hilo.
Naye afisa ushirika mkoa wa morogoro Bi,Esther Kisiga amewaomba wajumbe kuyatekeleza yale yaliyoadhimiwa kwenye kikao na kuwaomba vijana kuwa mstari wa mbele kujiunga katika vyama vya ushirika ili kujipatia maendeleo na amewatoa wasiwasi wakulima kuwa masoko yapo hivyo amewahimiza kujitahidi katika kilimo.
Kwa upande wake mjumbe wa chama cha  wakulima wa pamba Tanzania[TACOGA] Bi,Zena Kabonga amewaomba wanakilosa kulima zao la pamba na kuiomba serikali kuhusu pembejeo za kilimo hasa madawa kwani kuna baadhi ya dawa si nzuri haziui wadudu hivyo kusababisha kuendelea kuharibu mazao yao.

No comments:

Post a Comment