Thursday, November 25, 2010

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWEKA AWEKA MIPANGO YAKE KATIKA KUTATUA KERO ZA MAJI.

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWEKA AWEKA MIPANGO YAKE KATIKA
KUTATUA KERO ZA MAJI.


Siku Moja Baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji Katika Baraza Jipya La Mawaziri lililotangazwa Hapo tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka wa 2010 Mbunge Mteule wa Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Ameweka Bayana Mipango yake katika kutatua Kero za Maji Wilayani Njombe.

Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Mchana leo Mhandisi Lwenge Amesema Baada ya kuteuliwa Kuwa Naibu Waziri wa Maji Wanategemea kuandaa mpango Mkakati wa kuboresha Miundombinu ya maji hatua ambayo amesema itasaidia kupunguza Kero hizo bila kusahau wakazi wa mkoa wa njombe ambako ndiko alikopata kura zilizomfikisha hapo alipo katika wizara hiyo kama naibu waziri.

Naibu Waziri huyo Amesema kwa kushirikiana na Mbunge wa Njombe Kusini Ambae pia ni Spika wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Bi Anna Makinda wanategemea kuunganisha nguvu zao ili kuweza kutatua Matatizo ya Wananchi wa Mkoa mpya wa Njombe kwa ukaribu na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano.

Amesema kwa Wilaya ya Njombe kufanikiwa kupata Mawaziri Wawili katika Baraza la Mawaziri ni hatua ya kihistoria ya kuelekea kutatuliwa kwa Kero na Matatizo mbalimbali ya Wakaazi wake na hiyo inaonyesha kwamba kuna watu wenye uwezo waliopo katika mkoa huu wa Njombe ambao ni mkoa moya na tayari umeishatoa viongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,na hivyo ni hatua ya kujivunia kwa wananchi wa mkoa huu wa njombe kwa kuweza kuwa na viongozi wa ngazi za juu kabisa seriukalini na hivyo wao kama viongozi ni jukumu lao kuwatumikia wananchi hao wa mkoa huo wa njombe.

Hata hivyo Mheshimiwa Lwenge amesema licha ya kuwa sasa yeye ni naibu waziri lakini sit u ni kwa wananchi wa mkoa huo wa njombe bali pia ni kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla ikizingatiwa kuwa yeye ndiye naibu waziri hivyo atakuwa na kazi kubwa ya kumpa Waziri wake katika wizara hiyo yale yote yanayotokea nchini katika wizara yake.

Akizungumzia Sura ya Baraza Zima la Mawaziri ambalo limejumuisha Mawaziri Takribani 24 Wapya na Wengine Tisa wa Zamani wakikosa Nafasi Mhandisi Lwenge Amesema Hakuna Ulazima kwa kila Mbunge kuwa Waziri bali anaweza kushiriki Shughuli za Serikali kupitia Idara Tofauti Ndani ya Bunge

Amesema kwa Yoyote aliefanikiwa kuwa Mbunge Angeweza Kuwa Waziri katika Wizara yoyote lakini kwa wale walioteuliwa ni kama Wawakilishi wa Watanzania huku akiahidi kutekeleza yale yote alioyahaidi katika Siku 71 za Kampeni

Pia ameongeza kuwa kwa wale ambao hawakuwa mawaziri wanayo nafasi ya kutoa matatizo yao katika bunge la jamuhuri ya muungano na hivyo isingekuwa rahisi kwa wote kuwa mawaziri hivyo kinachohitajika ni kushirikiana kwa lengo la kupeleka mbele taifa la Tanzania.

Aidha Naibu Waziri Lwenge Amesema Hoja zinazozushwa na Baadhi ya Wanasiasa kuhusu umuhimu wa Baadhi ya Wizara Amesema Hoja hizo Hazina uzito Kwani kila Wizara Ina Umuhimu wake Kwenye Jamii.

Mapema Asubuhi Leo Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa alinukuliwa na Moja ya Chombo cha Habari akisema kuwa Baadhi ya Wizara Hazina Umuhimu na kudai kuwa Zimeundwa ili kuwafurahisha Watu Fulani na kuitaja Wizara ya Utumishi wa Umma kuwa haina Umuhimu.

No comments:

Post a Comment