Tuesday, November 9, 2010

VYANDARUA KUGAIWA WILAYANI NJOMBE

KUTOKA KATIKA WILAYA YA NJOMBE.
VYANDARUA TUJIKINGE NA MALARIA.


Wananchi ambao hawakuandikishwa kupewa vyandarua Wilayani Njombe Mkoani Iringa wametakiwa kutolalamika pindi ugawaji vyandarua hivyo utakapo anza kwani idadi ya vyandarua vilivyofika ni vya walioandikishwa tu.

Rai hiyo imetolewa na Afisa mtendaji wa mtaa wa Melinze na Nazareth bwana EZEKIEL NJAWIKE akizungumza na Mwandishi wa Habari hii ofisini kwake juu ya ujio wa vyandarua hivyo katika mitaa yake.

Bwana NJAWIKE amesema kuwa Vyandarua alivyopewa katika maeneo yake,mtaa wa MELINZE amepewa jumla ya vyandarua 920 na mtaa wa NAZARETH amepewa jumla ya vyandarua 720 ambavyo ni idadi ya wananchi walioandikishwa,hivyo kwa wale waliohamia kipindi cha karibuni na wale ambao hawakuwepo wakati wa kuandikishwa ndio watakaokosa vyandarua hivyo.

Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya wizara ya afya juu ya ugawaji vyandarua hivyo vitaanza kusambazwa ifikapo November 12 mpaka 14 kwa muda wa siku tatu na kukamilika kwa zoezi hilo hivyo watakaoshindwa kufika kwenye vituo hivyo kwa siku zote tatu hawata weza kupata vyandarua hivyo.

Katika hatua nyingine amewata wananchi hao kufuata maelekezo yaliyoandikwa kwenye kuponi juu ya vituo vya kwenda kuchukua vyandarua hivyo,kwani atakayekwenda tofauti na kituo alichoandikiwa hawezi kupata vyandarua hivyo na kwa mujibu wa muda wa kuanza kugawa ni kuanzia majira ya saa mbili asubuhi mpaka majira ya saa kumi kamili za jioni.

No comments:

Post a Comment