Tuesday, April 16, 2013

NMB KANDA YA MASHARIKI YATOA MSAADA WA MADAWATI 38 YENYE THAMANI YA TSH MIL 2.5 KATIKA SHULE YA MSINGI MTYANGIMBOLE WILAYANI KILOMBERO

Zaidi ya
wanafunzi 80 wa darasa la nne na la
tano wa shule ya msingi ya
Mtyangimbole
iliyopo kijiji cha Ikule kata ya
Mngeta wilayani
Kilombero,wanasomea kwenye
banda la nyasi huku wakiwa
wamekaa chini.

HabariKwanza Blog imeshuhudia hali hiyo
wakati wa makabidhiano wa msaada
wa madawati
38 yenye thamani ya shilingi milioni
mbili na laki tano uliotolewa na
Benki ya
Nmb Kanda ya mashariki shuleni
hapo.

Akizungumzia
hali hiyo Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo bwana Emanuely Njavike amesema
kuwa wamelazimka
kufanya hivyo kutokana na shule
hiyo kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa
kwani vyumba
vilivyopo kwa sasa ni
viwili ambavyo vinatumiwa kwa
kupokezana kwa darasa la kwanza,la
pili,la tatu
na la sita.

Mwalimu Njavike
amesema kuwa hali hiyo
imewafanya
wanafunzi kutohudhuria masomo
kikamilifu kutokana na miundombinu
ya shule hiyo
kuwa mibovu hususan kipindi hiki
cha masika ambapo maji hujaa
katika vyumba hivyo na kuwafanya
wanafunzi hao kusoma katika
mazingira magumu na hatarishi.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha
Mtyangimbole Bwana Sangalufu John
Kibonde amesema
kuwa wananchi wa kitongoji hicho
walijenga maboma mawili mara
mbili na
yakabomoka kutokana na mvua za
masika
zinazoendelea kunyesha baada ya
serikali
kuchelewa kumalizia maboma hayo
hali inayowakatisha tamaa wananchi
kuchangia
ujenzi wa shule hiyo.
Shule ya
Mtyangimbole yenye wanafunzi 195
kuanzia
darasa la kwanza hadi la sita
inakabiliwa na upungufu wa vyumba
vitano vya madarasa na matundu
nane ya vyoo.

Hata hivyo maafisa wa benki ya NMB na Mbunge wa viti maalumu kupitia
Chama cha demokrasia
na maendeleo chadema Mheshimiwa
Suzan Kiwanga wamesikitishwa na
hali hiyo na
kusema kuwa shule hiyo inahitaji
msaada wa hali na mali ili
kuwanusuru watoto
hao wanaosoma katika mazingira
magumu na hatarishi

No comments:

Post a Comment