Friday, January 3, 2014

VIJANA WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI ILI WAPATE MIKOPO KIURAHISI



Mbunge wa jimbo la mikumi mkoani morogoro Abdulsalama Amer amewataka vijana waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mkopo wa pikipiki zitakazowawezwsha kujikwamua kiuchumi.
Abdulsalama maarufu kwa jina la sas gesametoa wito huo kwa vijana wa jimbo lake la mikumi wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha kitete msindazimapema wiki hii wakati wa ziara yake kwenye kijiji hicho kilichopo kwenye kata ya Ruhembe wilayani kilosa.
Sas gas amesema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na kampuni husika itakayotoa mikopo hiyo na sasa kinachosubiriwa ni vijana hao kuunda vikundi na kufuata taratibu zinazotakiwa ili waweze kukopeshwa.
Mbunge huyo amesema mikopo hiyo itawasaidia vijana hao kupata pikipiki na wataweza kuacha kuendesha pikipiki za matajiri wao na kuendesha za kwao kitu ambacho kitawasaidia kijikwamua kiuchumi.
Wakiongea vijana hao wamesema kuwa wanampongeza mbunge wao kwa jitihada hizo kwani watakapokopeshwa hizo pikipiki zitawasaidia kupata pesa na kuweza kutimiza ndoto zao za maisha bora kwa upande wao.

No comments:

Post a Comment