Thursday, April 20, 2017

KAYA 151 ZIMEATHILIWA NA MAFURIKO KATIKA KATA YA MVUMI WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGORO

Kaya takribani 151 zimeathilika na mafuriko katika kata mvumi wilayani kilosa mkoani morogoro mafuriko yaliyotokea alfajili ya april 20 mwaka huu na kuathili vitongoji viwili bomba kumi na mvumi A katika kata hiyo.
Akizungumzia hali halisi ya mafuriko hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilosa Kesi Juma Mkambala amesema mafuriko hayo yameathili kaya 151 na kati ya kaya hizo kaya 15 zimebomoka kabisa na wakazi kukosa mahali pa kuishi pamoja na taasisi mbili za serikali ikiwemo shule ya msingi mvumi A pamoja na ofisi ya kijiji kuvamiwa na mafuriko hayo.Ameongeza kwa kusema kuwa tayari serikali imetenga eneo kwa waathilika wa mafuriko hayo kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwapatia chakula huku kamati ya maafa ya wilaya ikiendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Akielezea chanzo cha mafuriko hayo mtendaji kata wa kata ya mvumi Aloyce izdoli amesema kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni mto kisangata kujaa maji na kupasua na kuingia katika makazi ya watu na maji kukosa mahali pakutokea kutokana na eneo hilo kutokuwa na kalavati la kupitisha maji kwa kuwa eneo hilo kuna barabara ya lami itokayo dumila kuelekea kilosa hivyo maji kushindwa kupita kwenda upande wa pili wa barabara.

Baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo Betha Magesa na Mashaka Rock wamesema kuwa athali walizozipata ni kubwa kutokana na mafuriko hayo kuingia ghafla na wao hawakuweza kuokoa vitu vyovyote katika makazi yao na baadhi yao kukosa mahali pakuishi kutokana na nyumba kubomoka na mazao kuingia maji.

No comments:

Post a Comment