Wednesday, February 19, 2014

WADAU MBALIMBALI WAHIMIZWA KUENDELEA KUTOA MISAADA KUWASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI MOROGORO.


Serikali Mkoani Morogoro imefanikiwa kujenga mahema 330 katika vijiji viwili vilivyoathirika na Mafuriko katika wilaya ya Kilosa na Mvomero, ambavyo ni Magore na Mateteni, huku lengo la serikali likihitaji kujenga mahema 520 ili kumuwezesha kila wananchi kuwa na sehemu yake ya kuishi.


 Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera alipokuwa anapokea misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirka hao kutoka kwa wafanyabiashara mkoani humo (TCCIA) wakishirikaana na baadhi ya mikoa wanachama ambayo ni Njombe, Lindi,Mtwara, Manyara na Arusha.

 Pia Bendera amewatoa hofu wananchi kuhusu suala la kuibiwa kwa misaada inayotolewa na wadau mbalimbali kutowafikia walengwa kwa kukanusha mbele ya waandishi wa habari kuwa jamabo hilo halipo na halitaweza kutokea mkoani humo kwani misaada yote inayotelewa ni kwa ajili ya waathirika tu wa mafuriko hayo.

 Pia amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kwa wingi kuweza kuwasaidia waathirika hao ambao bado wanahitaji misaada mbalimbali na kuwasifu wafanyakazi wote kwa umoja wao wa kujitolea kuwasaidia waathirika hao.

Wanyabiashara hao mkoani humo wakishirikiana na baadhi ya wanachama kutoka mikoa jirani wametoa misaada mbalimbali kama vile chakula na Mavazi yenye thamani ya shilingi Millioni 5.5 kwa waathirika hao wa mafuriko katika wilaya ya Kilosa na Mvomero yalitokea january 22 mwaka huu na kuwaacha wananchi katika wakati mgumu.

No comments:

Post a Comment