Monday, March 17, 2014

MAFURIKO YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA KILOSA



Wakazi wapatao 228 wa kata ya magomeni kitongoji cha manzese wilayani kilosa wameathiliwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali.

Akithibitisha kutokea kwa mafuriko hayo mwenyekiti wa kitongoji cha masanze Abdul Bona amesema kuwa mafuriko hayo yameingia siku ya jumamosi  ya tarehe 15 march mchana na kusema kuwa wakazi wa eneo hilo wameathiliwa sana kwa mafuriko hayo kwa baadhi ya nyumba kubomoka na nyingine kuingiliwa na maji,Pia amesema kuwa tofauti na maji kuingia kwenye makazi ya watu mafuriko hayo yameathiri mazao pamoja na mashamba.

Aidha mmoja kati ya waathilika wa mafuriko hayo Said mandundu amesema kuwa nyumba zilizobomoka ni nyumba za udongo ambaye naye ni mmoja wao aliyekosa mahali pa kuishi na kwa sasa akiwa amehifadhiwa na jirani yake.

Kwa upande wake mzee kambi kamtande ambaya naye ameathiliwa na mafuriko hayo amesema kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni kutokana na mto mkondoa kutokuwa na muelekeo maalum na baadhi ya wakulima kulima pembezoni mwa mto huo.Pia amesema kuwa mafuriko hayo yameharibu mazao pamoja na mashamba kuingiliwa na mchanga ambao haufai kwa kilimo.

No comments:

Post a Comment