Tuesday, March 18, 2014

SHULE ZA MSINGI WILAYANI KILOSA ZANUFAIKA NA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA[BRN]



Mkuu wa shule ya msingi kilosa town wilayani kilosa mkoani morogoro mwalimu Edna Dungumaro ameupongeza mradi wa matokeo makubwa sasa [BRN]Kwa kuweza kuinua kiwango cha ufaulu katika sekta ya elimu.

Hayo ameyasema march 18 alipotembelewa na habarikwanza shuleni hapo na kusema kuwa kwa upande wa shule yake kwa mwaka jana 2013 matokeo yalikuwa mazuri kwa kufaulisha wanafunzi 67 kati ya wanafunzi 71 wa darasa la saba na kueleza kuwa changamoto inayomkabili katika shule hiyo ni wanafunzi kuwa watoro,Pia amesema kuwa shule yake imeshika nafasi ya kumi [10]kiwilaya.

Aidha Navy kareen Ndoeka ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo ya kilosa town ameushukuru mpango huo wa matokeo makubwa sasa [BRN]Kwani wameweza kupata elimu kwa kiasi kikubwa.

Naye Jaspine mswaki mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo ya kilosa town ameupongeza mpango huo mwa matokeo makubwa sasa [BRN]Pia amewaomba walimu kuendelea kuwafundisha kwa moyo ili wapate elimu iliyo bora.

No comments:

Post a Comment