Monday, March 24, 2014

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 11 ALAWITIWA WILAYA MVOMERO MKOA MOROGORO



Kijana mwenye umri wa miaka 21 Mkude Kulubuko anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi tangini.Tukio hilo limetokea katika kijiji cha tangeni kata ya mzumbe, tarafa ya mlali , wilaya ya mvomero mkoani morogoro ambapo mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo march 21 mwaka huu.
Akielezea tukio hilo babu wa mtoto aliye lawitiwa Charles Golaga amesema kuwa march 21 mwaka huu mjukuu wake alikuwa akicheza na watoto wenzake ndipo mtuhumiwa alipomrubuni na kwenda kumfanyia mnyama huo vichakani .
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha tangeni Joseph Peter ameeleza kuwa amedhibitisha kuwa mtoto huyo amelawitiwa baada ya kumpelekwa hospitalini na daktari kuweleza kuwa mtoto huyo amearibika sehemu zake za haja kubwa na anamatatizo ya kujisaidia ovyo.
Aidha  baba wa mtoto huyo John Kesi Gabriel amekili kwa kutokea kwa tukio hilo ambaye amesema mwanae anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa morogoro na hali yake anaendelea vizuri.
Aidha kwa upande wa Kamanda wa Polisi mkoa  Morogoro Faustine Shilogile alipotafutwa kulizungumzia tukio hilo amesema kuwa hana taarifa zozote kwani yupo kikazi nje ya mkoa morogoro.

No comments:

Post a Comment