Thursday, March 13, 2014

WILAYA YA KILOSA KUNUFAIKA NA MLADI WA MAJI VIJIJINI.


Wakazi wa wilaya kilosa mkoani morogoro watanufaika na mradi wa maji safi na salama ifikapo june 2014 chini ya benk kuu katika vijiji kumi wilayani kilosa. 

 Mradi huo unagharimu takribani milioni 801 ukiwa na lengo la kuboresha maji vijijini ambapo kwa wilaya ya kilosa mradi huo utanufaisha vijiji vya tundu,msowero,iwemba,mabwegele,dumila,zombo lumbo,lumango,kifinga na mikumi.

Akizungumza na wanakijiji wa mabwelebwele march 13 mhandisi wa maji wilayani kilosa Hosea Mwingizi  amewataka wanakijiji kutoa ushirikiano katika ujenzi wa mradi huo na kuwafafanulia mambo mbalimbali juu ya mradi huo ambapo kwa kijiji cha mabwegele kuna ujenzi wa visima viwili 

Aidha katibu  katika kijiji cha mabwegele SOLOMON Ibrahimu ameupongeza mradi huo kwa kuwapatia fursa hiyo ya kuwapatia maji na kusema kuwa kijiji chao chenye wanakijiji 4600 hakina bomba hata moja na kuushukuru sana mradi wa benk ya dunia
Aidha mwandishi msimamizi wa mradi huo Leornad Msenyele amewaelimisha wanakijiji wa mabwegele juu ya mpango wa mradi huo wa maji katika ujenzi wake hadi utakapo kamilika 

Pia mhandisi wa maji wilayani kilosa Mwingizi amewataka wananchi hao kutumia vyanzo hivyo vya maji vizuri pindi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment