Tuesday, May 20, 2014

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA ELIMU KATIKA KUANZISHA SHULE

Mkaguzi mkuu wa shule wilayani kilosa Ally Abdulhaman amewataka wadau wa elimu kufuata kanuni na taratibu za kuanzisha shule pamoja na vyuo.

Ameyasema hayo ofisini kwake wakati akizungumzia usajili wa Snai Media school iliyopo manzese wilayani kilosa na kusema kuwa shule hiyo haikusajiliwa tangu ilipoanzishwa mwaka 2009 na kusema kuwa walishatoa maelekezo kwa mmiliki wa shule hiyo kuwa ataje usajili wa shule hiyo mapema na kuongeza kuwa shule hiyo iliamuliwa kufungwa na mkaguzi wa mkoa mnamo tar 31 january lakini shule hiyo bado inaendelea kutoa mafunzo hayo ya elimu.

Aidha amesema kuwa wahisani hao huanzisha shule hizo kwa kupitia ofisi ya ustawi wa jamii yaani child care lakini ndani yake hutoa elimu ambapo ni kinyume na taratibu na sheria na kubainisha kuwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi 4 ndio wanaotakiwa kuwa kwenye child care na wanapofikia umri wa miaka 5 huyo anakuwa na umri wa kuanza elimu ya awali.

Naye mkurugenzi wa Snai media school Mery Paul Komba amesema kuwa shule yake ipo kwenye mchakato wa kuisajili likini pia amesema kuwashule hiyo bado ipo chini ya ustawi wa jamii na wapo kwenye mpango wa kuisajili lakini serikali inawapelekesha haraka na wanashindwa cha kufanya kwa sababu wanachanganywa na kuongeza kuwa swala la kufungwa kwa shule hiyo limewaumiza sana wazazi wenye watoto katika shule hiyo na kueleza kuwa elimu wanayoipata watoto katika shule hiyo ni nzuri na wanaumizwa wanapooona shule hiyo inataka kufungwa.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa lengo la kuanzisha shule hiyo ni kutokana na kuona kiwango cha elimu kinashuka na changamoto kubwa na swala la lugha ya kiingereza.

Nao wanafunzi katika shule hiyo ya Snai media school shurut palma na careen fredy wamesema kuwa changamoto inayowakabili shuleni hapo ni kutokuwepo maji kalibu pia vyoo kutofanyiwa usafi ulio sahihi kwa usalama wao.

No comments:

Post a Comment