Umoja wa katiba ya wananchi [UKAWA]Wameendelea kuwahamasisha
wananchi juu ya umuhimu wa katiba na ukawa walivyojitoa kwenye bunge maalum la
katiba wakipinga mabadiliko yanayotarajiwa toka kwa kamati na kanuni,wakidai
kuwa yanaenda kinyume na azimio lililopitishwa na bunge hilo kwa kuleta maridhiano.
Akiongea katika mkutano ulioitishwa na UKAWA katibu wa chama
cha CUF wilayani kilosa Sudy muhombolage amesema kuwa sababu ya ukawa kujitoa katika
bunge maalum la katiba ni Lugha za kibaguzi,Vitisho vilivyojitokeza katika
bunge maalum la katiba pamoja na kuchakachua kwa rasimu ya katiba kwa baadhi ya
wajumbe wa bunge hilo la katiba.
No comments:
Post a Comment