Friday, May 16, 2014

SHIRIKA LIISILO LA KISERIKALI PARALEGAL CENTER LATOA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU WILAYANI KILOSA



Shilika lisilo la kiselikari morogoro paralegal center kwa ufadhili wa shirika la Legal Fund [LSF]Limehitimisha mafunzo ya kisheria kwa muda wa siku tano tangu May 12, 2014 hadi May 16, kwa watu 25 wilayani kilosa lengo likiwa ni kutoa mafunzo msaada wa kisheria kwa jamii masikini ambayo haiwezi kumudu gharama ya wakili.

Baada ya mafunzo hayo naibu wa wasaidizi wa kisheria wilayani kilosa[kilosa paralegal Association]Wilfredy Sumari amewataka wahitimu wote waliopata mafunzo mafunzo hayo ya haki za binadamu kujituma katika kutetea haki za wananchi hasa waishio vijijini na kuongeza kuwa anawaomba wananchi kuwapokea vizuri watetezi hao na kuwatumia kwa sababu wapo kwa ajili yao.

Nao baadhi ya wahitimu hao wa mafunzo ya kisheria ya haki za binadamu Sophia Paul,Ramadhan Hassan,Stella Venus na Henry Lembele wamelipongeza shirika hilo kwa kuwapatia elimu hiyo na kusema kuwa waliyofundishwa ni hali halisi ambayo ipo kwenye jamii na wameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wananchi,Pia wamezungumzia baadhi ya mafunzo waliyoyapapata ni pamoja na Ukatili wa kijinsia,Wosia,Talaka pamoja na dhana ya ndoa hizo ni mada chache kati ya walizojifunza zinazoisumbua jamii na jamii kutotambua haki yao kwa kuipata.

No comments:

Post a Comment