Friday, May 2, 2014

MAJAMBAZI YAPORA NA KUJERUHI WILAYANI KILOSA



Wafanyabiashara  wa mazao pamoja na nguo mnada wa Lumuma wilayani kilosa mkoani morogoro may 1 wametekwa na kuporwa mali zao na kujeruhiwa katika eneo la la mlima wa vua shati uliopo barabara ya lumuma wilayani kilosa.
Wafanyabiashara hao waliotekwa akiwemo Blai jaston na David Daudi komba wametekwa katika mlima wa vua shati na majambazi waliokuwa wakitumia silaha aina ya mapanga na Nondo,Kati ya bidhaa zilizotekwa na majambazi hao ni pikipiki aina ya sanlg yenye namba za usajili T 210PVA Iliyokuwa ikimilikiwa na msafiri mkazi wa mpwapwa na bidhaa nyingine zilizotekwa ni pamoja na nguo sambamba na maharage.Akielezea tukio hilo mmoja wa mateka hao bw,jaston amesema kuwa walitekwa may 1 majira ya saa 3 usiku eneo la mlima wa vua shati na kufungwa kamba za mpira na kuamrisha kutowaangalia usoni na kuamrishwa watoe vitu walivyonavyo ikiwemo fedha walizopata katika mauzo waliyouza kwa siku hiyo na walipokataa ndipo walipoanza kupingwa na nondo na hatimaye kukatwa mapanga.
Aidha mmoja wa ndugu wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Baba Maria Okocha amesema kuwa eneo hilo walipotekewa ni sehemu mbaya kwani kuna mlima mkali na maporomoko na kusema kuwa nyia hiyo ni hatari kwani hakuna watu wapitao mara kwa mara na kuongeza kuwa majambazi hao waliangusha mti barabarani wakiwavizia watu wanaorudi kutoka mnadani.
Kwa mujibu wa kaka wa majeruhi Sita Komba amesema kuwa  mdogo wake aitwaye David alikatwa mapanga eneo la kichwa na walimpeleka wamempeleka hospital wakipitia polisi kupata PF3 Na kueleza kuwa kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibubu.
Naye kamanda mkuu wa wilaya ya kilosa SP Break M.Magesa [OCD]amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la vua shati kwa tukio la majambazi kupora pikipiki na mali za wafanya biashara hao na kutoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi ili kubaini wahalifu wanaojaribu kujiinua.

No comments:

Post a Comment