Saturday, May 3, 2014

WATANZANIA WATAKIWA KUKABILIANA NA RUSHWA



Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk Mohamed Gharib Bilal amewataka watanzania kuwa wazalendo na nchi yao kwa kufichua vitendo vya rushwa vinavyoendelea kukithili nchini.
 Ameyasema hayo katika uzinduzi wa mbio za mwenge uliozinduliwa rasmi 2may katika mkoa wa kagera wilayani bukoba  katika viwanja vya kaitaba wenye kauli mbiu isemayo Tujitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba bora  na kusema kuwa rushwa ni chanzo cha kufifia kwa maendeleo kwa kuathili kila sekta na kusema kuwa watanzania wote tushirikiane katika kutokomeza rushwa na kusema kuwa jukumu la kutokomeza rushwa si jukumu la Taasisi ya kupambana na kutokomeza rushwa TAKUKURU peke yake bali sote tushirikiane katika kupambana na rushwa .Pia ameeleza sababu ya rushwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili,tama ya kujilimbikizia mali na kukosekana kwa uzalendo.Na kutoa Rai kwa watanzania kuacha kutoa na kupokea rushwa na wanapoona vitendo hivyo walipoti taarifa mapema kwa mamlaka husika.
Naye Waziri wa habari vijana tamaduni na michezo Fenera Mkangara amesema kuwa mwenge wa uhuru ni tunu na ishara ya uhuru wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania pia amesema kuwa mwenge wa uhuru ni unatumika kuchochea maendeleo kwa wananchi kwani wananchi huamasishwa kubuni na kuandaa miradi mbalimbali ya kijamii na uchumi.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka huu mwenge wa uhuru utakimbizwa kwa siku 165 katika halmashauri za wilaya zote za Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kusema kuwa mbio hizo za mwenge zinatarajiwa kifikia tamati katika mkoa wa Tabora tarehe 14 October 2014 na atakayehitimisha mbio hizo za mwenge ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment