Wednesday, May 21, 2014

VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA WORLD VISION



Shirika la world vision lililoanzishwamwaka 1959 nchini marekani na kuingianchini Tanzania mwaka 1980 lenyelengo la kuleta ustawi wa motto kuwa na maisha mazuri, Afya njema na kumjua mungu , May 20 mwaka huu limetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vya vikoba wilayani kilosa.

Katika mafunzo hayo yaliyohudhuliwa na wajumbe kutoka katika vikundi mbalimbali katika kutoa mafunzo hayo wamewezeshwa jinsi ya kuendesha vikundi vyao na taratibu na kanuni za kufuata katika kuendesha vikundi vyao.
NayemenejawamradiwaUlaya ADP katikashirikala  world vision Mathias Mwingila amesema kuwa katika kutoa mafunzo hayo 

                             MWEZESHAJI AKITOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI KATIKA UKUMBI WA MANYOVU - KILOSA
Wanakumbana nachangamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanavikundi kudai posho wakati wanapoitwa kupewa mafunzo na kusema kuwa lengo la world vision nikutoa mafunzo ya kuweza kujikwamua kimaisha na kuleta maendeleo katika jamii.

Aidha ameongeza kuwa changamoto nyingine ni mapokeo hasi kwa baadhi ya wajumbe wakidhani kuwa world vision inaeneza dini ya kikristo kutokana na shirika hilo kuanzishwa na watu wa dini ya kikristo na amebainisha kuwa shirika hilo halipo upande wowote wakidini ila lipo kwaajili ya kutoa mafunzo ya kujikwamua kimaisha kwa wajasiriamali wadogowadogo.

 WANAVIKUNDI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA MAFUNZO .
Nameongeza kuwa mradi huo kwasasa upo katika tarafa ya ulaya na Magole na utachukua muda wamiaka kumi na mitano na mikakati waliyojiwekea nikuhakikisha wajasiriamali na wananchi kwaujumla wanapata maendeleo kwa haraka.

Pia mwezeshaji katika semina hiyo Agripina P. Mtende amewataka wanavikundi hao kuwa na nidham ya fedha pindi wanapokopa katika vikundi vyao. 



Baaadhi ya wanavikundi hao Mwanaharusi Athumani, Donard Kusema na Stamili Shabani Kiwanga wamesema kuwa wameshukuru kwa shirika hilo  la world vision kwa kuwapatia elimu hiyo juu ya uendeshaji wa vikundi vyao.

No comments:

Post a Comment