Wednesday, April 30, 2014

SERIKALI YATOA TANI 160 ZA CHAKULA NA SHILINGI MILIONI 60 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MULEBA MKOANI BUKOBA.


MBUNGE WA MULEBA KASKAZINI MHESHIMIWA MWIJAGE KUWASAIDIA WAPIGA KURA WAKE 

Serikali imetoa jumla ya tani 160 za chakula na fedha taslimu shilingi milioni sitini zimetolewa na Waziri mkuu Mizengo Peter  Pinda  kwa  waathirika wa mafuriko  yaliyotokea march 28  katika vijiji vya kata ya Ibuga Wilaya ya Muleba  Mkoani  Bukoba.

Vijiji vilivyoathiriwa na maafa  hayo makubwa ambayo yamesababisha nyumba takribani  150 kuezuliwa na upepo  na watu kukosa makazi na mazao kuharibika ingawa hakuna aliyekufa na kujeruhiwa  katika tukio hilo      

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika ziara yake Mbunge wa Jimbo  la Muleba kaskazini mheshimiwa Mwijage amesema amesikitishwa sana baada ya kupata habari hizo kwani ni mara ya pili kutokea kwa maafa hayo,  kwa kuwa maafa kama hayo yalishawahi kutokea mwaka 2012 hivyo amewapa pole wanakijiji hao na kuwataka kutokata  tama kwa hali hiyo.    

Mheshimiwa Mwijage amesema baada ya kutembelea vijiji hivyo amebaini karibu nyumba 150 zimeezuliwa na upepo  na  baadhi familia kukosa makazi pamoja na mazao kuharibiwa vibaya hivyo ametoa bahasha kwa kila muathirika akidai kuwa ina misumari ndani yake na kuwakilisha msaada uliotolewa na serikali ikiwa ni tani 160 za chakula na msaada kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na milioni 60 alizotoa kwa ajili ya kununua maharage kwa wanakijiji hao.    

Mwijage pia amewaahidi wanakijiji hao kuwa wataletewa mahindi ambayo  watauziwa kwa bei ya shilingi hamsini kwa kilo lakini pia ametoa misaada ya papo hapo kama fedha tasilimu kwa ajili ya malipo ya ada kwa wanafunzi walioshindwa kwenda shule kutokana na hali hiyo.Baadhi ya misaada mingine ni sare za shule,mabati kwa bahadhi ya wanakijiji ,na  kutoa tamko kwa wakuu wote wa shule kutokudai ada kwa wanavijiji hivyo mpaka itakapofika mwezi  November  mwaka huu na amechukua jukumu la kuwasomesha watoto wote waliofanya vizuri katika masomo yao ya kidato cha nne mwaka huu  .   
  
Akitoa angalizo kwa  wale ambao wamekuwa wakitumia maafa hayo kwa manufaa yao binafsi kwa kuomba misaada toka sehemu mbalimbali kwa kutumia jina la kijiji cha Buhembo bila kupata kibali maalumu kutoka katika uongozi maalumu  na kusema kuwa huo ni wizi na wenye tabia hiyo waache na kufuata utaratibu   unaohusika  
Wakipokea misaada hiyo nao wanakijiji wa vijiji vya kata ya Ibuga wamesema wanaishukuru  serikali kwa kuwapa misaada hiyo kwani wamekuwa katika hali ngumu sana na kumshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kuchukua jukumu la kuwasomesha watoto wao

No comments:

Post a Comment