Thursday, June 5, 2014

POLISI JAMII WILAYANI KILOSA WATAKIWA KUWA NA MAADILI KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI




Polisi jamii wametakiwa kuwa na uadilifu na uwaminifu katika utendaji wao wa kazi wanapokuwa kazini .
Ameyasema hayo mpelelezi mkuu wa makosa ya jinai  Wilayani Kilosa Peter Nsanto wakati akiwakabidhi vitambulisho polisi jamii 26 wa kikundi cha mapambano group katika kijiji cha ulaya mbuyuni kata ya ulaya wilayani kilosa.

Ameongeza kuwa amefarijika sana baada ya kuwaona polisi jamii hao wakiwa na nia ya kufanya kazi kwa kujitoa kwa nguvu zote  na kusema kuwa vitambulisho walivyopata vitawasaidia katika utendaji wao wa kazi pia amewaasa polisi jamii hao kuwa kioo kizuri katika jamii kwa kujiepusha na vitendo viovu na badala yake wawe mfano mzuri katika jamii .
Kwa upane wake kamanda msimamizi tarafa ya Ulaya Sir. Agent Mohamed wa kata ya Ulaya amesema kuwa kampeni hii ya polisi jamii imesaidia sana kupunguza mlundikano mkubwa wa kesi mahakamani  kwani kesi nyingi zitatatuliwa ngazi ya vijiji tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwa kila kesi kupelekwa polisi.

Aidha mtendaji kata , kata ya Ulaya Hassani Kutundumu amefarijika sana kwa vijana hao wa polisi jamii kwa kupatiwa vitambulisho hivyo na amewataka polisi jamii hao kufuata maadili na utaratibu walizofundishwa jinsi ya ukamataji salama.

Nao polisi jamii wao akiwemo kamanda wa kikosi hicho cha mapambano group Majuto Mgawile na Jamira Cosmas Kopa wamesema kuwa wanashukuru kwa kupatiwa vitambulisho hivyo kwani imewarahihishia katika utendaji wao wa kazi .
  

No comments:

Post a Comment