Kesi
dhidi ya mshukiwa mmoja anyetuhumiwa kumbaka msichana mmoja katika eneo la
Bumala Magharibi mwa Kenya imeahirishwa.
Mshukiwa mmoja kati
ya sita wanaodaiwa kumbaka na kumtupa katika shimo msichana huyo kwa jina Liz,
alifikishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka ya kumbaka na kujaribu kumuua
msichana huyo, katika kisa ambacho kimezua hasira na hamasa miongoni mwa
wakenya wa tabaka zote
Kinyume na kesi
zingine, kesi hii iliendeshwa faraghani huku mawakili wanaowakilisha pande
husika na maafisa wa mahakama ndio walioruhusiwa kuwepo mahakamani.
Afisa
kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu aliwaambia waandishi wa habari kuwa ni
mkubwa pekee ambaye anapaswa kuzungumzia suala hili, kutokana na uzito wake.
Mawakili
wa mshichana huyo wamesema kuwa wao waliamua kuomba kesi hiyo kuendeshwa
faraghani ili kumlinda mhusika ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18. Pia
uamuzi huo ulichukuliwa ili kuwapa wanaohusika Imani ya kutoogopa mtu yeyote.
Mwandishi
wa BBC ambaye yuko mjini Busia Robert Kiptoo, anasema kuwa kinyume na
ilivyokuwa Jumatatu wakati mamia ya watu waliandamana, leo hali ilikuwa shwari
huku jamaa na marafiki tu ndio waliofika mahakamani.
Liz
alitoa ushahidi wake leo asubuhi na kisha kuhojiwa nyakati za alasiri kuhusiana
na tukio hilo ambalo lilimuacha kama amelemazwa kabisa.
Washukiwa
wengine watano bado wanasakwa na polisi na duru zinasema kuwa wazazi wao
wamepewa ilaani kuwawasilisha washukiwa hao mahakamani.
Liz
inadaiwa alibakwa na wavulana sita Juni mwaka jana na kututwa katika shimo la
choo, hali iliyosababishia majeraha ambayo kwa sasa yamemlemaza.
Tangu
wakati huo wanaharakati wa kijamii wamekuwa wakishinikiza mkuu wa polisi nchini
Kenya kuhakikisha kuwa waliombaka Liz wamefikishwa mahakamani.
Hata
hivyho sakata hiyo ilichukua mkondo tofauti pale, ilipofichuliwa kuwa
waliombaka waliachiliwa huru na polisi baada ya kuadhibiwa kufyeka nyasi katika
kituo kimoja cha polisi.
Kesi
dhidi ya mshukiwa mmoja wa ubakaji wa msichana Liz na kumjeruhi vibaya nchini
Kenya imeahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Juni.
Kesi
ya Liz ilisababisha ghadhabu sana sio Kenya tu bali duniani kote hasa kwa
ambavyo polisi waliishughulikia.
Muungano
wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopinga dhuluma dhidi ya wanawake,
uliongoza waandamanaji ambao baadaye walikusanyika katika kituo cha mkuu wa
jimbo, Isaiah Nakoru.
Liz
alibakwa mwaka jana na kuachwa na majeraha mabaya mwilini mwake
Walimkabidhi
mkuu huyo nyaraka zilizotiwa saini kutaka Liz atendewe haki.
Waliotia
saini nyaraka hizo wanamtaka mkuu wa polisi kuwakamata washukiwa na kitendo
hicho cha unyama dhidi ya Liz ambao walimbaka na kisha kutupa mwili wake ndani
ya shimo lenye urefu wa futi 25 mjini humo.
Viongozi
wa maandamano wanasema kuwa idadi kubwa ya wasichana waliobakwa tangu kusikika
kwa kisa cha Liz wamekuwa wakienda kuwashitaki watuhumiwa kwa polisi.
Liz
alibakwa na wanaume sita ambao walimuwacha na majeraha mabaya kwenye mwili wake
kiasi cha kulazwa hospitalini kwa miezi kadhaa.
Mamake
Liz alikuwa miongoni mwa waandamanaji.