Mashirika ya umma na binafsi yameshauriwa kuwashirikisha
wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kufuatilia masuala ya
ubadhirifu uliopo katika maeneo yao na kuwajengea mazingira rafiki na vyombo
vya dola ili kufichua vitendo vya ufisadi bila hofu .
Mkuu wa Oparesheni maalum za jeshi la polisi SAIMON SIRRO
amesema hayo wakati wa kufungua mkutano wa wataalam wanaoshughulikia makosa ya jinai
na kugushi kutoka taasisi za fedha ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuokoa
rasilimali za nchi na kutoendelea kuporwa na watu wanaojali maslahi yao
binafsi.
Kutokana na tatizo la kugushi na wizi kwa njia ya mtandao
kuendelea kushamili nchini, wataalamu wanaoshughulikia makosa ya jinai ya
kughushi kutoka katika taasisi za kifedha wamekutanishwa mjini Morogoro
kujengewa uwezo juu ya kubaini mbinu mpya za ughushaji ukiwemo ule wa mitandao.
Shirika la Afrikan union linazishauri wizara ,
idara na taasisi zake , pamoja na mashirika ya umma na binafsi kuwalinda
wafanyakazi na wananchi wanaofichua taarifa za ufisadi badala ya kuwatishia na
kuwaona ni wasaliti.
Katibu mtendaji wa shirika linalojishughulisha na
uchunguzi wa makosa ya kughushi ASFE amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuwaongeza ujunzi na weledi watendaji hao.
Pamoja na kuwepo kwa hatua kali za kisheria kwa
wanaopatikana na hatia katika makosa ya wizi wa kugushi lakini bado wizi huo
umeendelea kuwepo hali inayofanya nchi kuendelea kuwa maskini huku baadhi ya
watu wakiendelea kujinufaisha kupitia njia hiyo ya haraka.
No comments:
Post a Comment