Wednesday, June 25, 2014

MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA GARI WILAYANI KAHAMA




Mkazi wa mjini Kahama Mkoani Shinyanga Ismail Mohamed-(47) ambaye pia alikuwa mwamuzi wa Soka, amefariki dunia  kwa kugongwa kisha kukanyangwa na Lori la mchanga wakati akiendesha baiskeli katika eneo la Bijampola mjini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya farajimfinanga.com Mmoja wa mashuhuda Kapambara Juma amesema  kwamba, chanzo cha ajali hiyo ambayo imetokea jana jioni ni mwendokasi wa Roli hilo Aina ya Fuso lenye no.T 161 AQR Mali ya Ndeleye Trans lilokuwa linaendeshwa kwenye barabra ya Lami iendayo nchi za Rwanda na Burundi.
Tukio hilo limetokea mwezi mmoja tangu ajali nyingine iliyomuua msichana ambaye hakujulikana, hali iliyosababibisha Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani humo kuahidi kuyaondoa mara moja magari makubwa yanayoegeshwa na kubana njia barabarani hapo.

Wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo wamehoji ahadi ya Jeshi la Polisi kuyaondoa magari hayo huku yakizidi kuongezeka kila siku na wala hakuna hatua zozote za utekelezaji zilizoweza kuchukuliwa.

Ofisa wa kikosi cha usalama barabarani aliyefika kwenye tukio hilo Thoma Muyonga alipotakiwa kuzungumzia malalamiko hayo amesema, Polisi kwa kushirikiana na serikali walikuwa wakikamilisha hatua za kuhamisha maegesho hayo kuyapeleka nyakato hatua ambayo imekwisha kamilika.

Jeshi la Polisi wilayani humo linamtafuta dereva wa lori hilo ambaye alikimbia baada ya kupata ajali ambapo mazishi ya mwili wa Marehemu Mohamed yamefanyika jioni katika makaburi ya waislamu yaliyopo mtaa wa majengo mjini kahama. 




No comments:

Post a Comment