Aliyekuwa diwani wa kata ya mkwatani kupitia chama cha
mapinduzi CCM Amina mwarabu amefariki usiku wa kuamkia june 19 mwaka huu.
Akuzungumzia kifo hicho mtoto wa marehemu Ally Nassoro
amesema kuwa mama yake alikuwa na maradhi ya moyo na kisukari ambayo yalikuwa
yakimsumbua kwa muda mrefu na ndiyo yanayosadikika kupelekea kifo chake.Na
amefafanua kuwa marehemu mama yake amefariki akiwa na umri wa miaka 62 na
ameacha jumla ya watoto wane [4]wanaume watatu na wakike ni mmojana wote hao
wanajitegemea.
Akiongea kwa niaba ya chama cha mapinduzi [CCM] wilayani
kilosa katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi Twaribu Kassim Kaberege amesema
kuwa wameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu alikuwa
mwenyekiti msaidizi katika baraza la wazee wilayani kilosa pia alikuwa
mwenyekiti wa vijana wilaya ya kilosa na amesema kuwa limekuwa pengo kubwa kwa
jamii ya kilosa na taifa kiujumla kwani marehemu alikuwa ni mpiganaji wa
maendeleo.
No comments:
Post a Comment