Polisi jamii wametakiwa
kuwa na uadilifu na uwaminifu katika utendaji wao wa kazi wanapokuwa kazini .
Ameyasema hayo mpelelezi
mkuu wa makosa ya jinai Wilayani Kilosa
Peter Nsanto wakati akiwakabidhi vitambulisho polisi jamii 26 wa kikundi cha
mapambano group katika kijiji cha ulaya mbuyuni kata ya ulaya wilayani kilosa.
Ameongeza kuwa amefarijika
sana baada ya kuwaona polisi jamii hao wakiwa na nia ya kufanya kazi kwa
kujitoa kwa nguvu zote na kusema kuwa
vitambulisho walivyopata vitawasaidia katika utendaji wao wa kazi pia amewaasa
polisi jamii hao kuwa kioo kizuri katika jamii kwa kujiepusha na vitendo viovu
na badala yake wawe mfano mzuri katika jamii .
Kwa upane wake kamanda
msimamizi tarafa ya Ulaya Sir. Agent Mohamed wa kata ya Ulaya amesema kuwa
kampeni hii ya polisi jamii imesaidia sana kupunguza mlundikano mkubwa wa kesi
mahakamani kwani kesi nyingi
zitatatuliwa ngazi ya vijiji tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwa kila kesi
kupelekwa polisi.
Aidha mtendaji kata , kata
ya Ulaya Hassani Kutundumu amefarijika sana kwa vijana hao wa polisi jamii kwa
kupatiwa vitambulisho hivyo na amewataka polisi jamii hao kufuata maadili na
utaratibu walizofundishwa jinsi ya ukamataji salama.
Nao polisi jamii wao akiwemo
kamanda wa kikosi hicho cha mapambano group Majuto Mgawile na Jamira Cosmas
Kopa wamesema kuwa wanashukuru kwa kupatiwa vitambulisho hivyo kwani
imewarahihishia katika utendaji wao wa kazi .
No comments:
Post a Comment