Mkazi
wa mjini wilayani kilosa aliyetambulika kwa jina la Abdallah Ramadhani
aliyekadiliwa kuwa na umri wa miaka 60 ambaye alikuwa mlizi wa ofisi za chama
cha mapinduzi ( CCM) wilayani Kilosa amekutwa amefariki usiku wakuamkia juni 12
mwaka huu
Akizungumzia
kifo hicho motto wa marehemu Ramadhani Abdallah amesema kuwa baba yake alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa shindikizo la damu na alipatiwa matibabu juni 9
mwaka huu na kuambiwa arudi juni 12 kwa matibabu zaidi, na ameongeza kwa kusema
kuwa marehemu baba yake ameacha watoto tisa na wake watatu.
Akifafanua
tukio hilo katibu wa chama cha mapinduzi Wilayani Kilosa Dodo Sambu amesema
kuwa mlinzi huyo ni kweli alikuwa akifanya kazi katika ofisi hiyo ila hawakuwa
na taarifa yoyote ya ugonjwa ya mlinzi huyo.
Kwa
upande wake mhudumu wa ofisi hiyo ya CCM wilaya ya kilosa Hamisi Ally ambaye
yeye analala ofisi hapo ameeleza kuwa yeye alipoamka asubuhi alikuta mwili wa
mlinzi huyo ukiwa umelala chini na kueleza kuwa katika ulalaji aliomkuta
alihisi kuwa amefariki.
Akithibitisha
tikio la kifo hicho hicho kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa
masale Dickson ameeleza chanzo cha kifo hicho kuwa ni tatizo la shindikizo la
damu lililokuwa juu sana na ndio lililompelekea kifo chake.
No comments:
Post a Comment