Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi( CUF)
Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro uliokuwa
ufanyike juni 15 mwaka huu umehairishwa kutokana na sababu mbalimbali hadi
utakapotajwa tena na Uongozi wa Wilaya.
Hali hiyo imejidhihirisha katika Ukumbi wa Manyovu uliopo
Wilayani Kilosa ambapo ndipo Uchaguzi ulipangwa kufanyika saa mbili usiku ili kuweza kuchagua Viongozi mbalimbali wa
Wilaya mara baada ya kushindwa kuhudhuria robo tatu ya wajumbe wa Chama hicho.
Kwa mujibu wa Mjumbe
wa Uchaguzi ngazi ya Taifa Husein Shaban Mwakikoti amesema kuwa mkutano huo
ulikusudiwa kuwa na wajumbe mia tatu lakini hadi kufikia saa tano usiku wajumbe
mia moja na ishirini tu ndio waliokuwa wamewasili,hali iliyosababisha
kuahirishwa kwa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho inayosema kuwa
Uchaguzi utafanyika kama kutakuwa na
nusu ya wajumbe wote.
Ameongeza kwa kusema kuwa sababu kubwa iliyosababisha wajumbe
kutohudhuria Mkutano wa Uchaguzi ni pamoja na ucheleweshwaji wa Taarifa kwa
wajumbe pamoja na umbali kulingana na jiografia ya wilaya ya Kilosa
kwani wajumbe wengine hawakufika kabisa .
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano huo wamemuomba
Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Husein
Mwakikoti kupeleka kwenye uongozi wa Taifa changamoto mbalimbali zilizoko ndani
ya Wilaya ya Kilosa ikiwemo Ruzuku ndogo ambayo haikidhi mahitaji ukilinganisha
na ukubwa wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment