Imeelezwa kuwa jamii ya kilosa
inaongoza katika kuwatumikisha watoto wadodo katika shughuli za kibiashara.
Akizungumzia utumikishwaji huo wa
watoto june 13 mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo ametoa tamko kwa wazazi
wote watakao bainika kumtumikisha motto shughuli za kibiashara atachukuliwa
hatua kali za kisheria na kuwataka viongozi vijiji,kata na Tarafa kusimamia
katika kusimamia katika kupatikana kwa haki za mtoto.
Naye Afisa ustawi wa jamii wilaya ya
kilosa Saidi kataluma amesema kuwa wilaya ya kilosa inaongoza kwa utumikishwaji
wa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na kueleza kuwa katika wilaya ya
kilosa maeneo yanayoongoza kuwatumikisha watoto katika shughuli za kibiashara
ni Mtendeni na Behewa na kuongeza kwa kusema kuwa wanajitahidi kutoa
elimu kwa jamii kutambua haki za mtoto na kuzifuata.
Kwa upande wa mwenyekiti wa
kitongoji cha behewa Zainobi Eusobio amesema watoto wengi wanatumikishwa
shughuli za kibiashara ni kutokana na hali ngumu ya kimaisha na kuwataka
wananchi kuwa na ushirikiano katika kutetea haki za watoto.
Kwa upande wake fikira mtolera mkazi
wa behewa ambaye ni baadhi ya wazazi wanaowapa kazi za kibiashara watoto
amesema kuwa wanafanya hivyo kutokana na hali ngumu ya kimaisha na kupelekea
kuwafanyisha kazi watoto hao na ameongeza kuwa serikali nayo haiwajali
kwani mara nyingi hupita kuwaandikisha majira katika familia zinazoishi
katika mazingira magumu na hatimaye kutowapatia muafaka wa kuwaandikisha majina
hayo.
No comments:
Post a Comment