Serikali wilayani Kilosa
imetaja miradi itakayo zinduliwa na mbio za mwenge mwaka huu ndani ya wilaya ya
Kilosa.
Akizungumzia miradi hiyo
juni 11 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo mnamo june 23 mwaka huu
mwenge utapokelewa ukitokea wilaya ya kilombero na kukiombizwa wilayani kilosa
, Ukiwa ndani ya wilaya ya Kilosa mwenge huo utazindua miradi saba ambayo ni
pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji mikumi uliyogharimu jumla
ya shilingi milioni mia nane , kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kukoboa ya
vijana ilakala, kuweka jiwe la msingi katika hosteli ya shule sekondari isanga , ufunguzi wa kituo cha kupima VVU ulaya .
Amesema miradi hiyo amabayo
imegharimu fedha nyingi ni lazima wananchi waakikishe inaendelezwa na si kufia
njiani kama inavyojitokeza katika baadhi ya miradi inayoanzishwa , kwani hayuko
tayari kuona miradi ikiteketea na kuona fedha za wananchi zikipotea bila kuleta
faida .
Mwenge huo utakimbizwa
ndani ya wilaya ya Kilosa kwa siku moja na utalala kata ya kisanga kabla ya
kukabidhiwa kwenye uongozi wa mkoa ambapo ndipo utakapo
kuwa mwisho wa mbio za mwenge katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro baada ya
hapo uongozi wa mkoa utaukabidhi mwenge huo mkoani Iringa .
Pia ametoa wito kwa wanaqnchi
wa kilosa kutoa michango ili kufanikisha mbio hizo kwani hadi kukamilisha mbio
hizo zinahitajika milioni 30 na kusema kuwa hadi sasa wamekusanya kiasi cha shilingi
milioni 15.
No comments:
Post a Comment