Watoto mapacha wenye umri wa miaka sita wamekufa baada
ya kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati wakicheza.
Kamanda wa polisi mkoa wa pwani Ulrchi Matei amesema
watoto hao wametumbukia kwenye kisima kilichojirani na nyumbani kwao ambapo
baada ya pacha wa kwanza kuona mwenzake anazama alikwenda na kutaka kumuokoa
ndipo naye alipozama.
Kwa mujibu wa kamanda huyo tukio hilo la june 8 mwaka
huu majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha pipani kiwangwa kata ya kiwangwa
tarafa ya msata wilaya ya bagamoyo.
Ameeleza kuwa miili ya watoto hao mapacha baada ya
kuopolewa ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko .
No comments:
Post a Comment