Monday, June 9, 2014

KILOSA WAPATA LISHE BORA



Shirika lisilo la kiserikali HUDESA june 9 mwaka huu limetoa mafunzo  ya lishe bora kwa mtoto  kwa vitendo kwa kina mama wa wilayani Kilosa. 

Naye  Mkaguzi wa shirika hilo la HUDESA Mkoa wa Morogoro Deus Ngerangera  amesema kuwa kufuatia mafunzo waliyopewa ili kuweza kunusurru maisha ya watoto kwa kupewa lishe bora na kuwataka wananchi kulima viazi vitamu vya njano kwa ajili ya kupata vitamin “A” pamoja na mboga za majani na kusema kuwa hawezi kukaa tena na kuongeza kuwa uji huo ni muhimu kwa ajili ya mtoto aliyetimiza miezi sita baada ya kuzaliwa.
                                     Mkaguzi wa shirika mkoa wa morogoro Deus ngerangera
Aidha katika mafunzo hayo ya kuandaa lishe bora kwa mtoto kina mama wilayani Kilosa wameweza kujifunza kuandaa chakula cha mtoto cha aina tatu ambapo ni uji wa mahindi , uji wa ulezi , pamoja na uji wa viazi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wilaya ya kilosa Antony Fuime ameeleza kuwa wilaya ya kilosa ipo kwenye ha;I mbaya katika lishe ya watoto kwa kusema kuwa ni wilaya ya mwisho ukilinganisha na wilaya nyingine katika mkoa wa morogoro.

                                       Mratibu wa shirika la HUDESA Antony Fuime
Nao maafisa lishe wilaya ya Kilosa Zainabu Waziri na Zaiba Kibona  wamewataka wamama wa wilayani Kilosa kuzingatia lishe hiyo waliyojifunza kwani itawajengea uwezo mzuri watoto kiakili na kiafya na kuongeza kuwa wazazi wanatakiwa kujishughulisha kwa kilimo kwa ajili ya kuwapatia hamu ya kula.

Kwa upande wao wamama waliopatiwa mafunzo hayo Joyce Chedgo (Mama Lucy) na Jeni Kigunda (Mama Elikana)  wamesema kuwa wameshukuru kwa kupatiwa mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi na kusema kuwa wao kabla ya kupatiwa mafunzo hayo walikuwa wanawapa vyakula watoto wao vya aina moja.
                                                                                                

No comments:

Post a Comment