Kituo cha usaidizi wa Kisheria Paralegal (KIPA) kilichopo Kilosa Mkoani
Morogoro kimepokea vitabu vya aina 3 vya usaidizi wa kisheria kutoka Kituo cha
Sheria na haki za Binadamu kwa kushirikiana na Twaweza lengo ni kuwaongezea
uwezo wa kujitambua wananchi kuhusiana na Katiba mpya na haki zao.
Akizungumza na HABARIKWANZA ofisini kwake Msaidizi wa Kisheria
wa Wilaya ya Kilosa Vimwaya Manyoli amesema kuwa wamepokea jumla ya vitabu elfu
ishirini na nne juni 22 mwaka huu ambavyo ni kitabu Katiba ni nini,Twende wapi
na Hashuki mtu hapa.
Amesema kuwa vitabu
hivyo ni vizuri kwani vinaelimisha Jamii na wananchi kwa Ujumla pia mtu anaweza
kuelewa kwa kuangalia picha zilizomo kitabuni humo na amewashauri wananchi kuwa na mazoea ya kujisomea vitabu ili waweze
kukuza uelewa wao wa Kimawazo.
Aidha ameongeza kuwa wananchi endapo watajenga mazoea na
kusema kuwa yaliyomo ndani ya vitabu hivyo yanasadifu maisha yaliyopo
sasa.
No comments:
Post a Comment