Wito umetolewa kwa Serikali kupanga bei maalumu kwa wakulima
itakayo weza kuleta tija pindi watakapo vuna mazao yao hali itakayo pelekea
kuepukana na bei za wafanya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wito umetolewa juni 24 mwaka huu na wananchi wa wilayani
kilosa wakiongea katika kitao walichokaa na waandishi wa habari kujadili mada iliyokuwa
ikisema ni kipaumbele gani kimetolewa kwa wakulima juu ya mpango wa matokeo
makubwa sasa (BRN).
Mmoja wa wananchi hao Skutoka Mgeta ambaye hatukuweza kupata
jina lake amesema kuwa bei wanayouzia
mazao yao inapangwa na wafanya biashara
kwani bei zao haziendani na
ghalama za uzalishaji hivo kushindwa kuendesha maisha yao na kubaki kuwa watu
wa maisha duni.
Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali inatakiwa kuweka mikakati
ya bei ya wakulima kama ilivyo kwa wafanya biashara ili waweze kuepukana na umasikini kupitia
kilimo.
Naye mchangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Mr Kipala
amesema kuwa Serikali iandae soko la kuuza mazao ya wakulima kwa urahisi.na
kwamba wasipoweka utaratibu mkulima atazidi kukandamizwa kwani mfanyabiashara
atanunua bidhaa kwa bei anayo itaka
kutokana na uwitaji wa mteja.
No comments:
Post a Comment