Saturday, June 14, 2014

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBIU YAO



Wito umetolewa kwa wananchi wa kata ya mbumi wilayani kilosa mkoani morogoro kuona umuhimu wa kutunza mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Ameyasema hayo Rajabu mhina june 12 mwaka huu wakati akizungumza na mwandishi wetu ofisi kwake kuwa kumekuwa na wananchi ambao hutupa taka hovyokatika mifereji jambo ambalo linasababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na malaria.
Mhina amesema hali hiyo ya utupaji taka hovyo inasababisha mifereji kuziba na kusababisha maji machafu kutuama kwenye makazi yao ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wanatakiwa kutunza mazingira bila ya kusubiri uongozi wa serikali kwani wanaoathilika ni wananchi wenyewe.
Aidha amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutunza mazingira pamoja na kufyeka nyasi na kuzibua mifereji ambayo imepita pembezoni mwa makazi yao ili kuepukana magonjwa ya mlipuko.
Pia ameiomba serikali kutoa elimu na msaada na vitendea kazi kwa wanainchi ili waweze kuzibua mifereji ambayo imeziba hususani ile yenye sentimeta 60 ili kuepukana na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment