Katika kukuza kiwango cha ufaulu
na kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa [BRN]shule ya msingi mazinyungu
imetoa zawadi kwa wanafunzi waloshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika
mhula huu wa kwanza ambapo June 6, 2014 mmwaka huu shule za msingi zimefunga
kwa likizo ya muda wa mwezi mmoja.
Katika utoaji wa zawadi hizo
mwalimu mkuu wa shule hiyo Lameck mkude amesema kuwa wametoa zawadi hizo kwa
wanafunzi walioshika nafasi hizo kwa ajili ya kuleta mwamko wa kukazana kusoma
kwa bidii kwa wale ambao hawakufanya vizuri kwa mhula huu wa kwanza.
Pia amesema kuwa tatizo la
kushuka kwa kiwango cha ufaulu shuleni hapo ni pamoja na utoro wa rejareja na
baadhi ya wazazi kuwapa wanafunzi kazi za kibiashara muda wa masomo na baada ya
masomo na amewataka wazazi kuachana na dhana hiyo ya kuwafanyisha kazi watoto
na badala yake wawatengee muda wa kujisomea.
Aidha mwalimu wa taaluma wa
shuleni hapo Isaya mlimi amesema kuwa katika kukuza kiwango cha ufaulu shuleni
hapo wameibua mbinu ya kuwataja wale wanafunzi kumi dhaif walioshika nafasi ya
chini na wale wanafunzi bora walioshika nafasi ya juu lengo likiwa ni
kuwahamasisha wale ambao hawakupata alama nzuri za ufaulu.
Kwa upande wao wanafunzi
waliopata alama za chini yaani wale kumi dhaifu wamesema kuwa sababu iliyowapelekea
wao kutokufaulu ni kutopata muda wa kujisomea kwa kupewa kazi za nyumbani na
wanapomaliza huwa wanakuwa wamechoka na kushundwa kujisomea.
Aidha kwa upande wa wanafunzi
waliofaulu kwa wastani mzuri Abdalah chandafa,kwini Zuberi na Hasani Isumaili
wamesema kuwa wao wamefaulu vizuri kwa sababu walikuwa wanawasikiliza walimu
kwa umakini na kuongeza kuwa nidhamu nayo imewafanya kufanya vizuri katika
mitihani yao.
No comments:
Post a Comment