Wafanyabiashara wa soko la
sabasaba lililopo wilayani Kilosa Mkoani morogoro wamelilalamikia uongozi wa
CCM wilaya kwa kuwabomolea mabanda yao wanayofanyia biashara .
Wakizungumza hali hiyo ya
uvunjaji wa mabanda ya sokoni hapo Baadhi ya wafanyabiashara hao Juma Maliwa na
Mrisgo Samatta wamesema kuwa mabanda yao yamebomolewa hivi karibuni sababu ikiwa ni kupisha ujenzi wa Flame za
kibiashara ambapo wamedai kuwa flame hizo ambazo zitajengwa ni kwa ajili ya
watu binafsi . Na wamelalamika kuwa katika ubomoaji huo wafanyabiashara
hawakupewa muda wa kujiandaa kwa ajili ya kuhamisha bidhaa zao pia
hawakuandaliwa mazingira ya kuhamishia biashara zao hali iliyopelekea wateja kupata
usumbufu.
Naye katibu msaidizi wa
soko hilo la sabasaba Juma Kigoma amesema kuwa mpango huo wa bomobomo ulikuwepo
kwenye mpango na Lengo ni kuboresha hali ya soko hilo na kuongeza kuwa
wafanyabiashara hao walipewa muda na miezi sita kwa ajili ya kujiandaa.
Kwa upande wake katibu wa
chama cha mapinduzi wilayani Kilosa Twribu Kassimu Kaberege amesema kuwa
bomobomo hiyo ni kwa vipande ambavyo havina watu lengo likuwa ni kuboresha soko
hilo na kufanya wale ambao hawana nafasi ya kufanya biashara waweze kupata
nafasi hiyo katika soko hilo.
Aidha ametoa ametoa wote
kwa wito kwa wafanyabiashara wa soko la sabasaba wasifanyie biashara zao katika
vibanda ambavyo vimeezekwa kwa makuti na
badala yake wametakiwa kuezeka vibanda vyao kwa bati.
Na ameongeza kuwa hawajatoa
tanko la kuvunjwa kwa mabanda hayo ila waliwataka wafanyabiashara hao waviezeke
vibanda vya kwa makuti.
No comments:
Post a Comment