Wananchi wa wilayani kilosa
mkoani morogoro wameshauriwa kujiunga na mfuko wa bima ya Afya CHF ili
kupunguza gharama za maisha.
Ameyasema hayo mkuu wa
wilaya ya kiilosa Elias Tarimo June 16 mwaka huu kwenye maadhimisho ya mtoto wa
Afrika ambapo kiwilaya yamefanyika katika kata ya zombo kijiji cha nyali
yaliyobeba kauli mbiu isemayo KUPATA ELIMU BORA NA ISIYO NA KIKWAZO NI HAKI YA KILA MTOTO.
Tarimo amesema kuwa kwa
kutekeleza kauli mbiu hiyo mtoto anatakiwa kukua katika afya njema na
kuwashauri wazazi na walezi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya hiyo itasaidia
kupunguza gharama ya kimaisha kwa kuchangia shilingi elfu tano kwa kipindi cha
mwaka mzima na serikari itachangia mwanachama
shilingi elfu tano na kufikia shilingi elfu kumi.
Aidha amesema kuwa tatizo
la madawa kutopatikana mahospitalini ni kutokana na wananchi wachache kuchangia
mfuko huo wa Bima ya Afya CHF na serikali kushidwa kukidhi hitaji la dawa kwa
wananchi,Hivyo amewaomba wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili
kuondokana na tatizo hilo la upungufu wa madawa hospitalini.
Naye meneja wa Mfuko wa
Bima ya afya mkoa wa morogoro Bi,Rose Ongara amefafanua kuwa mwananchi anapaswa
kuchangia shiliongi elfu tano kwa kaya yenye watu kumi na kufafanua kuwa kwa hao watu kumi wote
watatibiwa kwa hiyo shilingi elfu tano kwa kipindi cha mwaka mzima na kueleza
kuwa ni sawa na shilingi mia tano kwa kila mmoja atatibiwa kwa mwaka na
kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo ili kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya.
No comments:
Post a Comment