Imeelezwa kuwa zaidi ya shilingi milioni kumi na sita
zimekusanywa katika maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru wilayani kilosa
mkoani morogoro kutoka sehemu mbalimbali wilayani humo.
Hayo ameelezwa na mwenyekiti wa kikao hicho cha kamati
ya sherehe za mwenge Elias Tarimo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kilosa
kilichofanyika wilani kilosa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashuri mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Aidha Tarimo amewataka wakuu wa idara na watendaji wa
kata kuwahimiza waliochini yao kuchanga michango hiyo ili kufanikisha sherehe
hizo za mbio za mwenge.
Amesema mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa june 23
mwaka huu ukitokea kilombero ukiwa umebeba ujumbe usemao” Katiba ni sheria kuu
ya nchi “wenye kauli mbiu isemayo JITOKEZE
KUPIGA KURA YA MAONI ILI TUPATE KATIBA MPYA ambapo utazindua miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ameongeza kusema kuwa miradi
itayofunguliwa na mwenge ni pamoja na Hostel ya sekondari ya Kisanga kituo cha
uhamasishaji wa kupima ukimwi ulaya na kuweka jiwe la msingi kwa kituo cha
wakulima Isanga.
No comments:
Post a Comment