Imeelezwa kuwa jumla ya watoto 863 wameripotiwa kufanyiwa
vitendo vya ulawiti huku wanaowafanyia hivyo wakiwemo ndugu zao wa karibu
na watoto 250 wametupwa na kutelekezwa
ambapo 142 wakiwa wametekwa na watoto 10 wamefanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam juni 16 mwaka huu na
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) Harold Sungusia wakati akizungumza kwenye
Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika na kuelezea changamoto mbalimbali zinazo
wakabili watoto.
Sungusia amesema kuwa kutokana na kukithiri kwa hali hiyo ya
ukatili dhidi ya watoto, ametaka Haki na Ulinzi wa watoto iwe ajenda ya kila
mdau hasa Wanasiasa kuifanya kitaifa katika mikutano yao.
Ameongeza kwa kusema kuwa wanasiasa wanapaswa kufanya hivyo
wakiamini kwamba itahamasisha wananchi kwa uzito mkubwa kutokana wao kuwa na
nafasi kubwa ya kusikilizwa na kuwafikia wananchi wengine kwa wakati.
Pia ameitaka Serikali iweke mikakati ya kiulinzi itakayo muwezesha mtoto
kujitambua na kujilinda mwenyewe kabla ya mtu mwingine na kuongeza kuwa wananchi kwa ujumla wanapaswa kuheshimu nafasi ya
watoto katika jamii na pale ambapo Haki zao zinakiukwa basi ni vizuri kutoa taarifa
katika sehemu husika.
No comments:
Post a Comment