Monday, August 25, 2014

RAIS KIKWETE AWATAKA WAFUGAJI KUWA WASTAARABU KATIKA MIFUGO YAO.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi wilayani kilosa kutowapokea wafugaji bila mpangilio kwani ndio sababu kubwa ya migogoro ya mara kwa mara wilayani humo.
Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete akiwa anaongea na wananchi wa wilayani kilosa mkoani morogoro.

Ameyasema hayo August 24,mwaka huu katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani kilosa mkoani morogoro ambapo amekagua mradi wa kufua umeme wa maji kisanga pia ameweka jiwe la msingi katika barabara ya kiwango cha lami kutoka Dumila hadi Rudewa.
Aidha Kikwete amesema kuwa viongozi wasiwe wakarimu kupita kiasi cha kuwakalibisha wafugaji wengi katika eneo moja na kusema kuwa mifugo inaongezeka lakini ardhi haiongezeki pia amezungumzia swala la wahanga wa mafuriko wa 2010 kuhusu kupatiwa viwanja kwa ajili ya makazi mapya ambapo amemhoji mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilosa kuhusu swala hilo na mkurugenzi kuahidi kuanza kulishughulikia zoezi hilo la ugawaji wa viwanja mwanzoni mwa wiki hii.
Wananchi waliokusanyika kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr,Jakaya Kikwete

Sambamba na hayo Rais kikwete amekumbana na changamoto nyingi za wananchi wa wilayani kilosa ambapo wananchi wa wilayani kilosa wanauhitaji wa maji safi na salama,barabara ya lami pamoja na umeme mambo ambayo ameyasema kuwa yapo kwenye mchakato.
Wakwanza kutoka kulia ni MKuu wa mkoa wa Morogoro John Bendera na wa kwanza kutoka kushoto ni mbunge wa jimbo la mikumi Sas ges.

Katika ziara hiyo ya Rais kikwete pia ameambatana na waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli ambaye naye ameongea na wananchi wa kilosa kuhusu ujenzi wa barabara ya lami itokayo Dumila hadi mikumi na kusema kuwa ujenzi huo wameugawa kwa awamu tatu awamu ya kwanza ni kutoka Dumila hadi Rudewa ambapo ujenzi huo tayari umeshakamilika na awamu ya pili ni kutoka Rudewa hadi kilosa na mwisho kutoka kilosa hadi mikumi.
            Mheshimiwa Jakaya kikwete akihojiana na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilosa

Aidha mbunge wa jimbo la kilosa Mustafa Mkulo amemuuomba Rais kikwete kukamilisha ujenzi huo wa barabara ya lami kwabla hajaondoka madarakani kwa ajili ya kuwapatia maendeleo wakazi wa wilayani kilosa.
                                            Wananchi wakitawanyika mara baada ya mkutano

Pia Rais kikwete amezawadiwa zawadi mbalimbali kutoka wilayani kilosa ikiwa ni pamoja na ng’ombe wawili majike na wote wanamimba na dume moja la ng’ombe,kinyago cha tembo kutoka TANAPA picha ambayo wamemchora Rais kikwete pamoja na mchele tani moja ambao unalimwa wilayani kilosa mkoani morogoro.

No comments:

Post a Comment