Saturday, August 23, 2014

VIONGOZI WAWA KIKWAZO KIKUBWA CHA MIMBA MASHULENI



Imesemekana kuwa tatizo la wasichana kupata mimba wakiwa mashuleni linasababishwa na viongozi  kutowafuatilia waliowakatisha masomo wasichana hao wakiwa bado wapo shuleni. 
              Bodi ya shulewa kwanza kushoto ni mratibu elimu kata akifuatiwa na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ukwiva Liberath patrick Ngure na kufuatiwa na mwenyekiti wa bodi ya shle Mussa Hamisi na wa pili kutoka kulia na ni Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael Mvulungu

Akizungumza katika bodi ya shule august 22 mwaka huu Mkuu wa shule ya Ukwiva Liberath Patrick Ngure amesema kuwa tatizo la wasichana kupata mimba shuleni hapo limekuwa sugu kutokana na kila mwaka kuongezeka kwa wasichana wanaopata mimba ambapo hadi kufikia February mwaka huu tayari wasichana wane walionekana kuwa na ujauzito na kufikia mwezi may msichana mmoja aligundulika kuwa ni mjamzito na kusema kuwa swala hilo kwa upande wake amewasilisha majina kwa Afisa mtendaji kata kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi lakini hakuna jitihada zozote zilizoonyeshwa kutoka kwa kiongozi huyo jambo ambalo ameeleza kuwa linamkatisha tamaa.
                                           Mwalimu mkuu wa shule ya ukwiva Liberath Patrick Ngure
Aidha ameongeza kuwa aliandika barua yenye kumbukumbu namba USS.CS.HM.VOL11/69 iliyokuwa ikihitaji taarifa juu ya mimba za wanafunzi wane [4]zilizoripotiwa katika  ofisi ya kata na mtendaji wa kata aliahidi kuleta namba za kesi zilizofunguliwa mahakamani jambo ambalo hajalitekeleza.
Kwa upande wake Afisa tarafa wa tarafa ya ulaya Raphael mvulungu amesema kuwa bodi ya shule inatakiwa kusimamia maswala ya kishule kwa makini ili kumpa nafasi mkuu wa shule kuweza kuendesha shule kwa makini kwa kubaki na swala la kukuza elimu shuleni hapo na si vinginevyo.

 
                                            Mjumbe katika bodi ya shule Crensensia Mfanyakazi
Wakichangia mada hiyo ya kuongezeka kwa mimba mashuleni baadhi ya wajumbe Mratibu elimu kata Robert Mshani,Crensensia Mfanyakazi wamesema kuwa viongozi ngazi ya kata wamekuwa wapuuziaji juu ya ufuatiliaji na utatuzi wa matatizo ya shuleni hapo jambo ambalo linakwamisha maendeleo shuleni hapo.
                                       Mjumbe wa bodi hiyo ya shule Rubanga Mapesi

Mwisho mwenyekiti wa bodi hiyo ya shule Mussa Hamisi kwa kushauriana na wajumbe wameamua kuunda kamati itakayowafuata viongozi wanaoonyesha kukwamisha swala la ufuatiliaji wa kufungua kesi mahakamani dhidi ya wale wasichana waliopata mimba.
 Mwenyekiti wa bodi ya shule Mussa Hamisi

No comments:

Post a Comment