Saturday, August 23, 2014

RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA DARAJA LA MTO KILOMBERO

Wananchi wa wilayani kilombero mkoani morogoro watanufaika na barabara itokayo Ruaha wilayani kilosa hadi Ifakara wilayani kilombero.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la mto kilombero.
Pia rais kikwete amezungumzia shabaha ya serkali kuwa na viwanda kumi vya sukari na kusema kuwa mchakato unafanyika ili kupata hekta laki mbili na nusu kwa ajili ya uwekezaji huo.
Wakati huohuo Rais Kikwete amefungua mradi wa umeme katika mji wa mwaya unaofadhiliwa na REA ambapo tayari zaidi ya vijiji ishirini na saba 27 vinanufaika na mradi huo sambamba na kujionea mfumo mpya wa matibabu ujulikanao kwa jina la TELMEDICINE katika kituo cha afya cha mwaya mfumo huo unasaidia kutoa matibabu kwa wataalam ambao watakuwa katika kituo kingine kwa kumpatia mtaalam anayetoa matibabu maelekezo ya nini afanye kwa mgonjwa hasa upasuaji.
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,  Alhamisi, ya Agosti 21, 2014, ameweka historia nyingine katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro wakati aliposafiri kwa treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ikiwa ni mara yake ya kwanza kutumia usafiri huo katika kipindi chake cha Urais.
Rais Kikwete, akifuatana na Mama Salma Kikwete, amesafiri kilomita 143 ndani ya Behewa la Kirais (Presidential Coach) la T-One kwa kiasi cha saa tatu na dakika 25 akitokea stesheni ya Ifakara katika Wilaya ya Kilombero kwenda Stesheni ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro vijijini.
Baada ya hapo Rais kikwete anatarajiwa kuwasili wilayani kilosa august 24 mwaka huu siku ya ijumapili na atazindua miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa umeme katika kata ya kisanga na kuzindua barabara ya lami kutoka Dumila wilayani kilosa hadi Rudewa wilayani kilosa na kufuatiwa na kuongea na wananchi wa wilayani kilosa.

No comments:

Post a Comment