Tuesday, August 19, 2014

WAKULIMA WILAYANI KILOSA WAILAUMU SERIKALI KWA KUWAPOKEA WAFUGAJI AMBAO WANAHARIBU MAZAO YAO

Wakulima wa wilayani kilosa mkoani morogoro wailalamikia serikali kwa kutowajali kutokana na mifugo kuingia kiholela wilayani humo na kuharibu mazao yao mashambani mwao.  
                     wananchi wakiwa kwenye majadiliano kwenye mkutano juu ya usuluhishi wa kuvamiwa na mifugo kijijini hapo
Wakizungumza katika mkutano wa kijiji august 19 mwaka huu baadhi ya wakulima wa kijiji cha ulaya mbuyuni Timotheo Mahembula,Saidi Hamisi na Zena kondo Wamesema kuwa wanapata manyanyaso kutoka kwa wafugaji hao kutokana na kulishiwa mazao yao mashambani na viongozi kutotoa msaada wowote kwao,na wameongeza kwa kusema kuwa tarehe 12 august ya mwaka huu walikaa kikao na kuahidiwa na Afisa Tarafa Raphael Mvurungu kuwa baada ya siku saba [7] watapatiwa majibu sahihi juu ya mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji hicho lakini haikuwa hivyo kutokana na siku hiyo ya saba viongozi hao kutoonekana katika mkutano huo  wa wakulima.
                            Mifugo ikiwa shambani ikishambulia mazao aina ya mbaazi
Wameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa hawana Imani na viongozi wa kijiji chao kutokana na viongozi hao kushindwa kuwaondoa wafugaji katika kijiji chao na kutowasikiliza wakulima kuhusu kilio chao cha mifugo kuingia mashambani na kula mazao yao. 

Aidha kwa upande wake Afisa tarafa wa Tarafa ya Ulaya Raphael Mvulungu amesema kuwa yeye hakufika katika kikao hicho kutokana na tatizo hilo kuendelea kulitafutia ufumbuzi Zaidi na uliosahihi na ameongeza kuwa wananchi waondoe hofu kwani mgogoro huo utakwisha na wakulima wataendelea na shughuli zao kama kawaida kikubwa amewataka kuwa na mvumilivu katika kupa suluhu juuu ya tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment