Tuesday, August 5, 2014

VIONGOZI WILAYANI KILOSA WATAKIWA KUSIMAMIA WAFUGAJI KUTOINGIA KIHORELA WILAYANI KILOSA



Mkuu wa wilaya ya kilosa Elias Tarimo amewataka viongozi  wa vijiji kutowapokea wafugaji  wanaotoka maeneo ya vijiji vya  jirani na kuvamia katika maeneo ya wakulima.
Ameyasema hayo agost  4 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima wilayani kilosa mkoani morogoro na kusema kuwa katika wilaya yake kuna wafugaji wengi hivyo hahitaji tena wafugaji kutokana na wilaya hiyo kuwa na wafugaji wengi na kukwamisha shughuli nyingine za kimaendeleo.
Ameongeza kwa kusema kuwa viongozi waliopo vijijini wanawakaribisha wafugaji hao kwa kupewa rushwa na wanapoona mambo yanawashinda  huchukua hatua ya kuwafukuza na na kushindwa kutokana na rushwa ambayo wameshaipokea.
Pia amesema kuwa pindi atakapo baini kuwa kiongozi yeyote amepokea rushwa kwa ajili  ya kumkalibisha mfugaji katika eneo lake basi atakuwa amepoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa kilosa kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji kwa ajili ya kulinda ardhi na pia kuondoa migogoro.

No comments:

Post a Comment