Sunday, April 27, 2014

MASHINDANO YA MAIMOSI MKOANI MOROGORO KITAIFA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI MOHAMED ABDULWAKILY AWAPONGEZA FABIAN NA MARIAM KWA USHINDI WA MBIO NDEFU KATIKA MAIMOSI KITAIFA MKOANI MOROGORO (CROSS COUTRY)

MASHINDANO  YA  MAIMOSI  MKOANI  MOROGORO  KITAIFA:

Na Jonathan  Tossi - Jeshi  La  Polisi.

Katibu  mkuu wa  wizara  ya  mambo  ya  ndani  nchini  Mohamed  Abdulluwakily   amewapongeza  wanamichezo wa  wizara  hiyo  na kuwaaasa kuwa   michezo  nisehemu  ya   kazi  hivyo  waendelea  kushiriki  michezo  hiyo  kwa  hali na  mali. Pia  amesema  kinachoitajika  sasa  ni kuunda  timu moja kutoka idara  za  wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  nchi   na kuwa  na   timu  moja  ya  wizara.


Aidha  kwa mara  nyingine tena Wizara  ya  mambao  ya  ndani  ya nchi  imeendelea  kufanya   vema  katika  mbio  ndefu  za  umbali  wa  kilomita   kumi    zilizo  fanyika  nje  kidogo  ya  mkoa  wa morogoro katika  Barabara  ya   Dar  es    salaam  na   Zambia   majira  asubuhi   ya  leo  toka  kijiji  cha   Mindu   mpaka  Kijiji  cha   Rombo  umbali wa  kilomita  kumi   washiliki  katika   mashindano  hayo  ni  wizara   mambo  ya  ndani, wizara  ya  uchukuzi  Idara  ya  Polisi  ,Uhamiaji   na  Kampuni  ya  TTPL ya   Mkoani  morogoro
Washindi  katika   mbio  hizo    ni  wizara   ya  mambo  ya ndani  ambayo  imewakilishwa    na  wakimbiaji  wakimataifa   Fabian  Frank   na  Mariam  Abubakali   huku   Fabiani  akiibuka  mshindi wa  kwanza   na  Mariam  kuwa  mshindi  wa  kwanza   kwa  wanawak.

Aidha  katika  michezo  mingine   ya  bao  karata   na  drafti  wizara  ya  mambo  ya  ndani  inaendelea  kufanya  vema  katika  michezo  hiyo  huku mchezo  wa  drafti  ukiendelea  muda  huu katika  viwanja  vya  jamhuri  hapa  morogoro
 Pia  katika   michezo  ya  netball yaani mpila  wa  pete  timu ya  mambo ya  ndani  inashuka  ndimbani  hapo kesho  majira  ya  saa tisa  za mchana  kwa  mchezo wa  huo.

No comments:

Post a Comment